Header Ads

Responsive Ads Here

Serikali Yampeleka India Mtoto Anayeongezeka Uzito


unnamed
Mtoto Antonia Justine Msoka akitoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuelekea nchini India kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Kushoto ni mama yake, Salome Manyirizu Kisusi ambaye anamsindikiza. Wengine ni mwandishi na mpiga picha wa TBC.
 
A
Baadhi ya wauguzi na madaktari  wakimpandisha kwenye ambulance Mtoto Antonia kwa ajili ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Mwalimu Julius Nyerere leo.
A 1
Gari ya kubebea wagonjwa ikiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Mwalimu Julius Nyerere.
A 2
 
Mtoto Antonia akiwa amepumzika kwenye gari ya kubebea wagonjwa leo kabla ya kupanda ndege kuelekea India.
…………………….
 
 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), LEO imemsafirisha mtoto, Antonia Justine Msoka anayeongezeka uzito kwenda India kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
Mtoto Antonia mwenye umri wa miaka 17 alikuwa amelazwa Muhimbili tangu Novemba mwaka jana na kuanza kupatiwa matibabu.
Akizungumzia afya yake, Antonia amesema kuwa afya yake inaendelea vizuri na amewashukuru madaktari na wauguzi wa Muhimbili kwa kumpatia matibabu.
 “Nashukuru kwa msaada kwani sasa naenda Hospitali ya India kwa matibabu zaidi, naishukuru pia serikali kwa kunisadia,” amesema mtoto Antonia.
Awali Antonia alifikishwa Muhimbili akiwa na uzito wa Kilo 250, lakini sasa zimepungua na kufikia kilo 230.
Mama wa mtoto huyo, Salome Manyirizu Kisusi ameishukuru wizara hiyo kwa msaada fedha za matibabu na kumsafirisha kwenda India kwa ajili ya matibabu zaidi.
“Nawashukuru watu waliokuwa wakiniombea na pia wote walionichangia fedha za matumizi, Mungu awabariki. Pia, nawashukuru madaktari, wauguzi na uongozi wa Muhimbili kwa ushirikiano mzuri walionipatia,” amesema Mama Salome.  

No comments