Header Ads

Responsive Ads Here

SERIKALI: AWAMU YA 3 YA REA KUVIFIKIA VIJIJI, VITONGOJI NA MAENEO YA PEMBEZONI MWA NCHI.


6701-Mhe.kalemani
 
Na Nuru Juma,MAELEZO,DAR ES SALAAM
 
 
SERIKALI kupitia mradi wa awamu ya 3 ya usambazaji wa umeme vijijini (REA) imekusudia kusambaza umeme katika vijiji, vitongoji vyote, taasisi za umma na maeneo ya pembezoni mwa nchi ikiwemo visiwa.
 
Hayo yamesemwa leo bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani alipokua akijibu swali la Mbunge wa Bukoba Mjini (CHADEMA) Wilfred Rwakatale.
 
Dkt. Kalemani amesema kupitia mradi wa REA, Serikali inatarajia kukamilisha usambazaji umeme vijijini mwaka 2020 hadi 2021, na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco)  inaendelea kusambaza umeme maeneo yote ya mjini ambayo hayajapata nishati ya umeme.
 
“Baadhi ya vijiji ambavyo vipo ndani ya mamlaka za miji vinapelekewa umeme na shirika la Tanesco na bei ya Tanesco na REA ni tofauti kwani kwa mteja wa awali wa Tanesco hulipia 177,000 na REA hulipia 27,000””, alisema Mhe.kalemani.
 
Kwa mujibu wa Kalemani amesema Serikali bado inaendelea kujiridhisha na kuangalia ni vijiji gani vinastahili kupelekewa umeme kwa mradi wa REA ili kuhakikisha kuwa malengo ya mradi yanaweza kufikiwa katika muda uliopngwa.
 
Dkt. Kalemani ameongeza kuwa wakati wa uzinduzi mradi huo ulianza na mikoa 10 na walibakisha mikoa 15 kwa Tanzania bara na hadi sasa wamemaliza utaratibu wa kuwapata wakandarasi watakaojenga miundombinu ya mradi huo katika mikoa yote nchini.
 
Aidha Dkt. Kalemani amesema wakati wowote kuanzia sasa Serikali inatarajia kuwapangia vituo vya kazi na wakandarasi hao.
 
Aliwataka makandarasi hao kufanya kazi kwa bidii katika mikoa yao ili kuhakikisha  wanamaliza kazi zao kwa wakati na umeme unapatikana katika vijiji vyote bila kubagua nyumba.
 
Katika swali lake la msingi, Mbunge huyo alitaka kufahamu mikakati ya Serikali ya kusambaza umeme katika baadhi ya vijiji vilivyopo katika baadhi Wilaya za Mkoa wa Kagera.
 
Utekelezaji wa mradi wa Rea wa wamu ya 3 umeanza tangu Machi 2017 na unatarajia kukamilika mwaka 2021.

No comments