Header Ads

Responsive Ads Here

SERENGETI BOYS YANYOOSHA NJIA YA AFCON U17 GABON, YAIBANJUA CAMEROON GOLI 1-0


ser1
Timu ya Taifa ya Vijana U17 Serengeti Boys imefanikiwa kuifunga timu ya Taifa ya Vijana U17 ya Cameroon katika mchezo wa kirafiki uliochezwa mjini Yaunde Cameroon usiku huu ambapo mchezaji wa timu ya Serengeti Boys Ally King’azi ameifungia timu hiyo katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Akizungumza kwa njia ya Simu Mtangazaji wa Kituo cha Redia cha EFM Bw. Maulid Kitenge ambaye alikuwa shuhuda wa mchezo huo amesema vijana wa serengeti Boys wamecheza vizuri kama walivyoomyesha mchezo mzuri katika michezo ya awali na leo pia walionyesha kiwango kizuri cha mchezo na ndiyo maana wenyeji Cameroon pamoja na kwamba walikuwa nyumbani lakini wamelala goli 1-0 jambo ambalo linastahili kupongezwa na kila mtanzani kutokana na kujituma kwa vijana wetu Serengeti Boys.
Timu ya Serengeti Boys imeonyesha uwezo mkubwa katika michezo mbalimbali iliyocheza iwe ya mashindano au ya kirafiki ambapo hivi karibuni imeweza kufanya vizuri katika michezo yake kwa kutoka sare ya magoli 2-2 kwenye uwanja wa Taifa na timu ya taifa ya  Vijana ya Ghana, ikaifunga timu ya taifa ya vijana ya Gabon  2-0 mara mbili na leo imeweza kuifunga timu ya taifa ya vijana ya Cameroon 1-0 nyumbani kwao hili ni jambo la kuwapongeza vijana wa Serengeti Boys kutokana na uwezo wanaouonyesha katika mchezo.
Baada ya Mchezo wa leo Serengeti Boys itaelekea nchini Gabon kwa ajili ya kambi tayari kwa kushiriki michuano ya AFCON U17 inayotarajiwa kuanza mwezi Mei tarehe 14 na kama timu hiyo itafanikiwa kushinda michezo miwili tu basi itakuwa imekata tiketi ya kushiriki michuano ya Kumbe la Dunia kwa vijana (World Cup U17) itakayofanyika nchini India kuanzia tarehe 6–28 mwezi wa 10/ 2017 ikishirikisha timu 24.

No comments