Header Ads

Responsive Ads Here

SAMATTA ATUPIA KRC GENK IKIIBUTUA EUPEN MCHEZO WA EUROPA LEAGUE GROUP B


samsataaaaaaaa
Baada ya ukame kumuandama, Mtanzania Mbwana Samatta ameamka baada ya kuifungia timu yake ya KRC Genk bao la ushindi,Samatta amefunga bao la pili wakati Genk ikiigaragaza Eupen kwa mabao 2-1 katika mechi ya ya kutafuta timu itakayocheza Europa League msimu ujao.

Nahodha huyo wa Taifa Stars alifunga bao hilo katika dakika ya 28 baada ya kupokea pasi ya Thomas Buffel, akaupita msitu wa mabeki kwa kasi kabla ya kuukwamisha mpira wavuni.
Kabla ya hapo, Genk ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Jere Uronen katika dakika ya 18 akiunganisha basi nzuri ya Samatta hata hivyo Eupen walipata bao la kufutia machozi dakika ya 76 likifungwa na Mnigeria Onyekuru
Kwa ushindi huo, Genk inaendelea kuongoza Kundi B hatua ya play-off ikiwa na pointi 19 na kufuatiwa na Lokeren yenye ponti 10.

No comments