Header Ads

Responsive Ads Here

RONALDO AIMALIZA ATLETICO MADRID UEFA CHAMPIONS LIGI NUSU FAINALI YA KWANZA


3FDFD18400000578-4467182-image-m-62_1493756654097
Hattrick yake ya 7 katika michuano ya Champions League imemfanya Cristiano Ronaldo aifikie rekodi aliyokuwa nayo Lioneil Messi katika mashindano hayo ya UEFA.

Cristiano Ronaldo alikuwa mwiba mchungu kwa Atletico Madrid kwani mabao matatu aliyofunga, moja kipindi cha kwanza na mawili kipindi cha pili yalitosha kuiangamiza kabisa Atletico Madrid.
Real Madrid wanaendeleza ubabe wao kwa Atletico Madrid katika michuano ya Champions League kwani toka mwaka 1958 Atletico Madrid hawajawahi kuitoa Real katika mchuano hiyo.
Matokeo hayo yanaiweka Real Madrid katika nafasi kubwa kucheza fainali ya Champions League msimu huu kwani mechi ya pili itawabidi Atletico kuwafunga Real mabao manne ili wafudhu.
Katika mchezo huo Atletico Madrid walionekana kupwaya sana kwani hadi kipindi cha kwanza kinaisha walikuwa hawajapiga hata shuti moja kuelekea langoni kwa Real Madrid.
Atletico watawakaribisha Real wiki ijayo kujaribu kubadili matokeo haya ya mwanzo, leo inapigwa nusu fainali ya pili ambapo Monaco wataikaribisha Juventus.

No comments