Header Ads

Responsive Ads Here

RC TABORA ATAKA WAHISANI KUSAIDIANA NA TANZANIA KATIKA UTOAJI WA ELIMU YA URAIA KWA RAIA WAPYA WALIOKUWA WAKIMBIZI.

Na Tiganya   Vincent-Tabora
19.5.2017
Mkuu wa Mkoa Bw. Aggrey Mwanri ametoa wito kwa wadau ,Mashirika ya Kimataifa na Umoja wa Mataifa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha Watanzania wapya waliopewa uraia wa nchi hii wanapata elimu ya uraia ili wajue nini maana ya kuwa raia wa Tanzania na hatimaye waweze kuishi kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.
Bw. Mwanri alisema hayo jana mjini Tabora wakati alipokutana na Ujumbe wa Mabalozi wa Umoja wa Ulaya walikuwa kwenye  ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali na Ulyankulu ili kuangalia jinsi wanavyoweza kusaidia katika zoezi kuwaunganisha raia hao wapya na raia wengine.
Alisema kuwa Watanzania hao wapya hajui nini maana ya kuwa raia , hivyo ni vema wakaelimishwa kuhusu Katiba na Sheria mbalimbali zinatumika hapa nchini ambazo nao wanatakiwa kuzifuata na kuzitii kama wanavyofanya raia wengine.
Bw. Mwanri alisema kuwa elimu hiyo itasaidi kuwaunganisha raia hapo wapya na wengine ili waweze kuishi vizuri kwa kutii na kuheshimu Sheria za Tanzania na kujiona wao sio tena wakimbizi bali ni raia.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza  amekuwa akiwasisitiza Watanzania hao wapya kuishi nchini kama walivyo Watanzania wengine  na sio kuishi kama wanavyotaka wao au kwa taratibu za nchi nyingine.
Bw. Mwanri alisema kuwa amekuwa akiwaeleza wazi kuwa mtu yoyote aliyepata bahati ya kupata uraia wa nchi hii akitumia bahati hiyo vibaya na kusababisha uvunjifu wa sheria za nchini atakuwa anajiondelea ya sifa ya kuendelea kuwa Mtanzania na hivyo ataishauri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ajili kuangalia uwezekazo kufuta uraia wake .
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora aliwaeleza mabalozi hao kuwa Makazi hayo yanakabiliwa na uhaba wa huduma za jamii kama vile maji, afya na miundombinu.
Kwa upande wa Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Mhe.Roeland van de Geer alisema kuwa baada ya kujionea mazingira ya Makazi ya Ulyunkulu wao kama Umoja wa Ulaya wataenda kujipanga kwa ajili kuangalia ni eneo gani wanaweza kusaidia kwa ajili ya kupunguza matatizo yanayowakabili Watanzania hao wapya.

No comments