Header Ads

Responsive Ads Here

RC SHINYANGA,AFANYA ZIARA NA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MAENEO YENYE FURSA WILAYANI KISHAPU


unnamed
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na ujumbe alioambatana nao akiwa katika shamba la mtama kijiji cha Busongo kata ya Mwamashele. Wengine pichani katikati ni Mkuu wa wilaya hiyo, Nyabaganga Taraba na Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika, George Kessy.

4
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akimuonesha Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya fursa za uwekezaji viwanda eneo la Uchunga. Wengine pichani kulia ni Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya hiyo, Mang’era Mang’era  
1
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) na Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba wakiangalia namna mzani wa kupimia choroko unavyofana kazi katika eneo la Mhunze.
2
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza ndani ya kiwanda kidogo cha kutengeneza bidhaa za ngozi zikiwemo viatu wakati wa ziara hiyo.
3
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na baadhi ya wafanyabishara akiwa katika eneo la Mhunze wakati wa ziara hiyo.
5
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiangalia viatu vilivyotengenezwa na kikundi cha Badimi wakati wa ziara hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amefanya ziara katika wilaya ya Kishapu na kutembelea na kukagua maeneo yenye fursa mbalimbali za uwekezaji viwanda.
Katika ziara hiyo Telack aliweza kutembelea vikundi vya wananchi wanaotengeneza bidhaa za ngozi, mbunifu wa mashine za kukoboa nafaka na wakulima wa zao la mtama kata ya Mwamashele.
Akiwa katika kata ya Kishapu eneo la Mhunze alitembelea wanakikundi cha Badimi na kujionea bidhaa mbalimbali za ngozi zikiwemo viatu kuwataka Watanzania kupenda bidhaa za nchini.
Akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa wilaya hiyo, Nyabaganga Taraba pamoja na viongozi mbalimbali alisifu jitiada za kikundi hicho huku akiwataka Watanzania kupenda bidhaa za ndani.
Kwa upande wao vijana hao walimhakikishia kuwa wanaweza kutengeneza viatu kw ajili ya mkoa mzima lakini wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa malighafi na mashine.
Mkuu wa wilaya, Taraba alisema halmashauri hiyo iko nao bega kwa bega na tayari imetenga fedha kiasi cha sh. milioni 18 katika mwaka ujao wa fedha ili kukisaidia kikundi hicho.
Katika ziara hiyo pia mkuu huyo wa mkoa alimtembelea mwananchi Daudi Nkende ambaye mbunifu wa mashine za kukoboa nafaka zikiwemo mtama katika eneo la Uchunga.
Telack alisema kuwa Serikali imefungua milango kwa wabunifu wa vitu mbalimbali na hivyo washiriki ili kuunga mkono jitihada zake katika kutekeleza Sera ya Viwanda.

No comments