Header Ads

Responsive Ads Here

RAIS WA UGANDA AIPIGIA CHEPUO SGR CENTRAL CORRIDOR


 WAFANYABIASHARA CHANGAMKIENI FURSA RELI YA “STANDARD GAUGE”
Kampuni za Yapi Merkezi ya Uturuki na Mota Engil ya Ureno zimewataka Wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi nchini kutengeneza bidhaa zenye ubora ili kampuni hizo ziweze kutumia katika Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Standard Gauge (SGR) unayotarajiwa kuanza kujengwa nchini.

Hayo yamesemwa leo na Meneja wa Mradi huo Mhandisi Maizo Mgedzi katika mahojiano ya ana kwa ana na Idara ya Habari – MAELEZO Ofisini kwake kwenye makutano barabara ya Reli na Sokoine Jijini Dar-es-salaam.
Kwa mujibu wa Gazeti la Monitor la nchini Uganda, likimkariri Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni hivi karibuni kuhusiana na ujenzi wa SGR, limesema kuwa bei elekezi ya tani moja ya Saruji kwa fedha za Kitanzania ni Shiingi Laki Tatu (300,000/=) sawa na Dola za Kimarekani 100, wakati kiasi hicho hicho cha Tani za Saruji nchini uganda zinauzwa fedha za Uganda Laki Sita (600,000/=) sawa na Dola za Kimarekani 180.
Aidha, gazeti hilo limeeleza kwamba, bei ya Nondo tani moja zinazotengeneza nchini Tanzania inanunuliwa kwa Shilingi milioni 2.4, sawa na dola za Kimarekani 680 ambapo Tani moja ya Nondo nchini Uganda inauzwa kwa fedha za Uganda Shilingi Milioni 2.47 sawa na Dola za Kimarekani 700.
Kwa mujibu wa Mhandisi wa Mradi huo nchini Maizo Mgedzi, kutokana na bei elekezi ya ununuzi wa nondo na saruji kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo muhimu kwa uchumi wa Tanzania, ni dhahiri Makampuni ya ujenzi wa reli hiyo yatalazimika kununua bidhaa hizo kutoka hapa nchini, jambo ambalo wazalishaji wanatakiwa kutengeneza katika kiwango bora kinachotakiwa.
Kutokana na hali hiyo, Mhandisi Mgedzi amesema, kwa Wazalishaji ambao ni waaminifu watakaoweza kutengeneza bidhaa zilizo bora, Kampuni hizo mbili za ujenzi kutoka Ureno na Uturuki zitanunua kwa wingi zaidi ili kuweza kukamilisha ujenzi wa reli hiyo.
Aidha, kutokana na mahitaji makubwa ya bidhaa hizo Wazalishaji hao watalazimika kuongeza uzalishaji huku Kampuni hizo zikiajiri nguvu kazi kubwa ya vijana katika ujenzi wa reli hiyo ya SGR. Amesema Mgedzi.  
Mhandisi Mgedzi amewasihi Wazalishaji wa bidhaa hizo wahakikishe wanafuata masharti ya Mkandarasi na Washirika wao kutoka Korea ili kujenga uaminifu na imani kwa Watanzania kuwa wanao uwezo wa kuzalisha bidhaa bora zaidi na kuondoa malalamiko na wasiwasi kwa baadhi ya Makandarasi wanaofanya kazi za ujenzi hapa nchini.
Kinyume na hapo kama watakuwepo wafanyabiashara wasio na nia njema watajipenyeza na kuleta bidhaa na vifaa visivyo na ubora, maana yake reli itakayojengwa itakuwa haina ubora na matokeo yake Serikali ya Tanzania itapata hasara na haitaikubaliana na matokeo hayo. Amesema Mgedzi.
Akitoa maelezo ya ujenzi wa reli hiyo Mhandisi Mgedzi amesema utahusisha kumimina nguzo za chini za zege ambazo zitahitaji mchanga, kokoto , saruji na nondo bora kabisa ili kuifanya reli kuwa madhubuti na imara.
Kuhusu ujenzi wa Vituo vya reli hiyo Mdandisi Mgedzi amesema “Vituo vitakavyojengwa vitakuwa tofauti na vituo vya Reli ya Kati kwa sababu vinahitaji kuwa na njia nyingi zaidi katika kila kituo kimoja”.
“Hii itarahisisha treni kuweza kubadilisha njia na pia kukata mabehewa kwa urahisi hususani kwa yale yanayotakiwa kubaki kituoni na mengine yaweze kuondoka bila kuzuiliwa. Hivyo, vituo vya reli hii vitahitaji eneo kubwa zaidi katika kila kituo ukilinganisha na eneo lililopo katika vituo vya reli ya kati”.
Ujenzi wa reli ya SGR ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli tarehe 12 Aprili, 2017 katika Stesheni ya Pugu. Aidha, Rais aliwaahidi wakazi wa Pugu kupewa kipaumbele katika kuajiriwa na kufanya kazi wakati ujenzi wa reli hiyo utakapoanza.
Serikali imewapa Wakandarasi walioshinda Zabuni ya ujenzi wa reli hiyo miezi 30 kuweza kukamilisha na kuikabidhi Serikali ya Tanzania. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo itaanzia mji Mkuu wa Biashara wa Dar-es-salaam hadi Morogoro wenye urefu wa kilometa 205 na itakamilika mwaka 2019. Ujenzi wa reli hiyo utagharimu fedha za Marekani Bilioni 1.2, sawa na fedha za Tanzania shilingi Trilioni 2.7 Asilimia 50 ya fedha hizo ni za ndani na Asilimia 50 ni mkopo kutoka nje.
Tanzania ni nchi ya nne Barani Afrika kujenga reli ya SGR inayoendeshwa kwa umeme, mafuta au gesi. Nchi zenye reli kama hiyo ni Ethiopia, Afrika ya Kusini na au Misri  Botwana.
Mradi wa Ujenzi wa reli hiyo una Washauri Elekezi waliobobea ambao ni Korea’s national railway operator Korail katika awamu ya kwanza ya ujenzi Dar-es-salaam – Morogoro. Washauri Elekezi wengine ni M/S Dong Myeong Engineering Consult, Architecture LTD, M/S Unitec Civil Consultatnt LTD-Tanzania, M/S Multi-Tech Consultants (PTY) LTD-Botswana, M/S SSF Incentelre AG-Germany, M/S D’Appolonia SPA-Italy na M/S Balaji RailroadSystes PrivateLTD-India.
Reli hiyo pia itajengwa kuanzia Dar-es-salaam hadi Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania yenye urefu wa kilometa 2561 ambayo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwaka 2019. Reli hiyo pia  inatajaiwa kujengwa hadi Mpanda ikitokea Tabora na Kigoma pembezoni mwa Ziwa Tanganyika.   

No comments