Header Ads

Responsive Ads Here

RAIS JACOB ZUMA WA AFRIKA KUSINI KUWASILI LEO NCHINI TANZANIA


indexAmani, Upendo, Umoja, Mshikamano, Bidii na Juhudi za Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli vyote kwa pamoja vimekuwa nguzo na chachu ya kuwaleta wawekezaji kutoka nje ya nchi na viongozi mbalimbali kuwa na shauku ya kufika Tanzania.
Nchi ya Tanzania imepata heshima ya kupokea ugeni wa Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Rais Jacob Zuma ambaye hapo leo usiku  tarehe 10/05/2017 saa 3 usiku akiwa na ujumbe wa watu 120 atawasili nchini kwa ziara ya siku mbili na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.

Ugeni huo utatanguliwa na ujumbe wa Mawaziri wasiopungua sita. Ambao wataungana na Mawaziri wetu katika kujadiliana namna gani ya kutumia fursa ili kujenga uchumi wetu na uchumi wa Afrika Kusini.
Mgeni wetu atapokelewa Ikulu siku ya Alhamisi ya tarehe 11/05/2017 saa 3:00 asubuhi ambapo atapigiwa mizinga 21 kama heshima ya mapokezi yake.  Napenda kuwapa tahadhari wakazi wote wa maeneo ya jirani na Ikulu kuwa kutokana na tukio hilo kwa muda huo wanashauriwa kuwa katika hali ya tahadhari hasa kwa walio na magonjwa ya mshtuko.
Katika ziara hiyo marais hawa wawili pamoja na mambo mengine watasaini Hati mbalimbali za makubaliano ikiwemo za ushirikiano katika sekta ya maji baina ya nchi mbili hizi, ushirikiano katika sekta ya uchukuzi na katika masuala ya Rasilimali ya Wanyama na Misitu.
Kama ilivyo kawaida yetu kwa Amani, Upendo, Furaha na Ukarimu tuliokuwa nao katika kuwapokea wageni wetu tuungane na Rais wetu siku ya Jumatano katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwl. Julius K. Nyerere International Airport – Terminal 1 kuwapokea wageni wetu.
Mgeni wetu anatarajiwa kuondoka hapa nchini siku ya Alhamisi ya tarehe 11/05/2017 saa 3 usiku.
Asanteni sana.
Paul C. Makonda.
    MKUU WA MKOA
    DAR ES SALAAM
       9/05/201

No comments