Header Ads

Responsive Ads Here

RAIS DK SHEIN AWAFARIJI WANANCHI WA JIMBO LA PANGAWE ZANZIBAR LEO


FAR1
Wataoto wa maeneo ya Nyarugusu Wilaya ya Mjini,Unguja wakimuangalia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani ) wakati alipofika katika shehia ya Nyarugusu, Jimbo la Pangawe kuwafariji na kutoa pole kwa wananchi walioathirika na Nyumba zao zilizobomoka kutokana na Upepo mkali uliotokea jana katika maeneo yao na kupelekea uharibifu kwa kung’oka mapaa ya Nyumba wanazoishi, wakati alipofanya ziara maalum leo,[Picha na Ikulu.]16/05/2017.

FAR2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (mbele) wakati alipofika katika shehia ya Nyarugusu, Jimbo la Pangawe leo alipofanya ziara maalum ya kuwafariji  wananchi ambao Nyumba zao zimepata athari ya kun’goka kwa mapaa   kutokana na Upepo mkali uliosabisha   na  uharibifu   huo jana, ambao  umepelekea kukosa pahala pa kuishi,[Picha na Ikulu.]16/05/2017.
FAR3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana na Vijana waliojitolea kutoa msaada kwa Wananchi wa Shehia ya Nyarugusu Jimbo la Pangawe waliopatwa na  maafa ya Nyumba zao kungoka Mapaa kutokana na Upepo Mkali uliotokea jana, alipofanya ziara maalum ya kuwafariji  wananchi hao leo alipofika kutoa mkono wa pole, [Picha na Ikulu.]16/05/2017.
FAR4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na  kuwasalimia Wananchi wa Shehia ya Nyarugusu Jimbo la Pangawe waliopatwa na  maafa ya Nyumba zao kung’oka Mapaa kutokana na Upepo Mkali uliotokea jana, alipofika   kuwafariji na kuwapa pole kutokana mtihani walioupata,alipokuwa katika ziara maalum  leo akiwa na Viongozi mbali mbali wa Jimbo hilo, [Picha na Ikulu.]16/05/2017.
FAR5
Miongoni mwa Nyumba zilizoharibika kutokana na Upepo Mkali ulitokea jana katika maeneo ya Nyarugusu Jimbo la Pangawe Mkoa wa Mjini Magharibi na kupelekea Wananchi kukosa maakaazi ya kuishi,hali hilo aliiyona Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani ) wakati alipofanya ziara maalum leo katika Shehia hiyo, [Picha na Ikulu.]16/05/2017.
FAR7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) alipokuwa akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Shehia ya Nyarugusu Jimbo la Pangawe waliopatwa na  maafa ya Nyumba zao kung’oka Mapaa kutokana na Upepo Mkali uliotokea jana, alipofika   kuwafariji na kuwapa pole kutokana mtihani walioupata,wakati alipofanya ziara maalum  leo akiwa na Viongozi mbali mbali wa Jimbo hilo, [Picha na Ikulu.]16/05/2017.
FAR8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akisalimiana na Nd,Abdalla Ali Mohamed Mwananchi wa Makondeko Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakati alipofika Nyumbani kwake akiwa ni miongoni mwa Wananchi waliopatwa na  maafa ya Nyumba zao kungoka Mapaa kutokana na Upepo Mkali uliotokea jana,Rais alifika katika shehia hiyo leo wakati alipofanya ziara maalum ya kuwafariji  Wananchi, na  kutoa mkono wa pole,(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud, [Picha na Ikulu.]16/05/2017.
……………………………………………………………………………..
Na Miza Kona-Maelezo -Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema Jamii ina wajibu wa kusaidiana pale yanapotokea matukio ya maafa ili kuweza kunusuru matatizo zaidi yanayoweza kujitokeza.
Amesema yanapotokea matukio ya maafa katika Jamii si muda muafaka wa kulaumiana bali ni muda wa jamii kushirikiana kikamilifu na Wahanga kwa kuwasaidia kwa hali na mali.
Rais Shein ameyasema hayo huko katika Shehia ya Pangawe alipotembelea na kuwafariji Wananchi waliopata maafa ya nyumba zao kutokana na upepo mkali uliotokea hapo jana.
Amesema maafa na matukio kama hayo hayaji kwa taarifa yoyote bali ni mipango ya Mungu na kuwataka wananchi waliopatwa na maafa hayo waendelee kuwa na subira.
 “Simanzi kubwa imetokea katika Mwezi wa Aprili na Mei kwa kunyesha mvua kubwa ambazo zilileta maafa huko Pemba na upepo mkubwa uliovuma jana ambao umeleta maafa makubwa kwa wananchi kukosa makaazi” alieleza Dkt Shein
Amesema matukio makubwa  ya maafa hutokea katika kipindi cha mvua za masika kwani kipindi hicho mvua hunyesha kubwa ambazo hupelekea kuathiri jamii.
“Tusilaumiane, tusiwabeze, tusiwacheke matukio haya yanaweza kumpata mtu yoyote, wakati wowote haya yote yamepangwa na Mungu,wananchi tusaidiane aliyenacho amsaidie mwenziwe” amesisitiza Dkt Shein.
Hata hivyo Dkt Sheim amesema Serikali ina jukumu la msingi la kuwatakia mema wananchi wake kwa kuwasaidia pale wanapopata matatizo na kuwaletea maendeleo kwa kuwapatia misada mbalimbali inayohitajika.
Aidha amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wa pamoja na uvumilivu waliokuwa nao kwa kuweza kusaidiana katika maafa hayo yaliyotokea.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud amesema kutokana matukio yaliyotokea jana tayari Serikali imeunda Timu ya wataalamu 15 kutoka Baraza la Manispaa kupita nyumba hadi nyumba kutathmini athari zilizotokea ili kutoa misaada inayohitajika kwa jamii.
Mapema Mbunge wa Jimba la Pangawe Shamsi Vuai Nahodha amewataka wananchi waliopata maafa kuwa na moyo  wa subira katika kipindi hiki kigumu hivyo serikali kushirikiana na viongozi inachukua juhudi kubwa za kuweza kusaidia wananchi walioathirika.
Upepo huo ulitokea jana majira ya saa 3.15 asubuhi ambao jumla ya nyumba 123 ziliathirika na upepo huo.
Miongoni mwa nyumba hizo shehia ya Kinuni nyumba 96,Shehia ya Mwanakwerekwe nyumba 26 na Pangawe nyumba 1.

No comments