Header Ads

Responsive Ads Here

OFISI YA MADINI MKOA WA GEITA YAMSIMAMISHA MWEKEZAJI WA KIGENI KUJENGA KIWANDA CHA KUCHENJULIA DHAHABU


Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Geita, Ali Said akizungumza ofisini kwake  juu ya hatua ya kumsimamisha mwekezaji kuendelea na ujenzi wa kiwanda cha kuchenjulia dhahabu . 
Wanakijiji  cha Ililika Kata ya Nyarugusu Wilayani Geita wakishirikiana kuziba Eneo la Bara bara ya kuelekea kwenye kiwanja ambapo ndiko ujenzi unaendelea.

Zikiwa ni siku Mbili zimepita tangu  wananchi wa Kjiji cha Ililika kata ya Nyarugusu
Wilayani Geita , kuandamana kupinga mwekezaji ambaye ni Raia wa China
kuweka kiwanda cha  kuchenjulia dhahabu katikati  ya makazi yao na karibu na
chanzo cha maji kijijini Hapo ,ofisi ya madini Mkoa wa Geita imemsitisha
mwekezaji kuendelea na shughuli za ujenzi kwenye eneo hilo.
Akizungumza Ofisini kwake na mtandao wa maduka online ,
Afisa  Madini Mkazi Mkoa wa Geita, Ali Said ameitaja kampuni ya wachina
iliyozuiliwa  kuwekeza Kiwanda cha
kuchenjulia dhahabu kuwa ni JIN XIN, ambayo inaubia na Mtanzania.
amesema kuwa kutokana na malalamiko ya wananchi walikwenda
kukagua na kujilizisha na kwamba wamemsimamisha mwekezaji kuendelea na mradi
huo kutokana na malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho.
 “Tulipata taarifa ya kuandamana kwa wananchi kupinga mradi
huo ambao mwekezaji anataka kuweka na sisi kama ofisi ya madini tumefika Kijijini
hapo kwaajili ya kujilizisha na kweli tumegundua eneo sio rafiki hivyo tumezuia
shughuli ya ujenzi kutokuendelea kwenye eneo hilo”Alisema Ali.
Katika hatua nyingine Afisa huyo amesema, mwekezaji yoyote
anayewekeza kiwanda cha kuchenjulia dhahabu ni lazima apate ridhaa ya wananchi
wa eneo husika.
“Kuna watu ambao wanashirikishwa kwenye swala la uwekezaji
naamini ni serikali ya Kijiji na wananchi hivyo nadhani ni muhimu wananchi nao
wakabariki kazi ambayo mwekezaji anaitaji kuweka nikiwa na maana ni swala la
ushirikishwaji”Alisema Ali. 
Kwa upande wake Mjiolojia kutoka ofisi hiyo ya madini Godfrey
Keraka, amebainisha madhara yakiwemo madhara ya kiafya ambayo yanaweza kuwapata
wananchi wa maeneo hayo pamoja na makelele ya kiwanda vikiwemo vyanzo vya maji
kuharibiwa.
Maduka Online imefika kwenye ofisi za afisa Mazingira wa Wilaya
Hiyo Bi,Helen Eustace ambapo amesema kuwa wao kama ofisi hawana taarifa yoyote
ya Mwekezaji Huyo na Kwamba wataakikisha wanafuatilia ili kuchukua hatua za
kiafya na kimazingira.

No comments