Header Ads

Responsive Ads Here

Mtu mwenye kilo 595 afanyiwa upasuaji kupunguzwa uzito

Binadamu anayesadikiwa kuwa mwenye uzito mkubwa kwa sasa duniani, amefanyiwa upasuaji wa kitaalam kwa lengo la kumpunguza uzito kwa karibu nusu.

Mtu huyo Juan Pedro Franco ambaye sehemu kubwa ya maisha yake amekuwa akikaa tu kitandani, amewahi kufikia uzito wa kilo 595.
Kwa mujibu wa Dakta Jose Castaneda wa Mexico, upasuaji huo wa kwanza umekuwa wa mafanikio na kuwa anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine mwezi Novemba mwaka huu.
Iwapo zoezi la upasuaji kwa mara ya pili litafanyika kwa mafanikio, tumbo la Franco litakuwa limepunguzwa na pia utumbo wake kutengenezwa.
Aliyekuwa akishikilia rekodi ya uzito duniani kwa kuwa na kilo 597 Manuel Uribe wa Mexico, alifariki mwaka 2007.
Naye Eman Ahmed Abd El Aty kutoka Misri, aliyeaminika kuwa mwanamke mwenye uzito mkubwa duniani, hivi karibuni alifanyiwa upasuaji kama huo nchini India.
Madaktari wamesema matibabu yake ambayo pia yalihusisha kuboresha mlo wake, yalimsaidia kupunguza kilo 323 kwa miezi mitatu, na kubakiwa na kilo 177 pekee.

No comments