Header Ads

Responsive Ads Here

MSUVA AUPELEKA USHINDI WA YANGA KWA YUSUF MANJI


manji.
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva amesema matokeo ya ushindi wanayoyapata uwanjani ni kwa ajili ya kumfariji mwenyekiti wa timu yao Yusuf Manji ambaye hivi karibuni alipatwa na matatizo.

Msuva amesema watapambana katika michezo minne iliyosalia ili kuhakikisha wanatetea taji lao na kupeleka furaha kwa mashabiki wa timu hiyo pamoja na Manji.
“Tunashinda ili kumfariji mwenyekiti wa timu yetu Yusuf Manji ambaye alikuwa na matatizo na kuwa pembeni kwenye masuala ya timu kwa muda,” Msuva amesema wakati akihojiwa na Mtandao wa Fullshangweblog mara tu baada ya kumaliika kwa mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons ambapo Yanga wameshinda 2-0.
“Tutapambana katika mechi nne zilizobaki ili kuhakikisha tunashinda taji la ligi na kupeleka furaha kwa mashabiki wetu wanaotuunga mkono pamoja na mwenyekiti wa timu.”
msuva-simon_1kqja8tnp4tui1pa2ux7txlil3
Msuva ambaye ameshafunga magoli 12 kwenye ligi amesema, mabadiliko yaliyofanywa na kocha pamoja na kufaanyia kazi marekebisho waliyopewa na kocha wao wakiwa mapumziko ndiyo ndiyo yaliyo zaa magoli mawili ya haraka.
“Mwalimu alishaona ugumu wa Prisons uko wapi, tulipokuwa mapumziko alitupa maelekezo pamoja na kutuambia tupite pembeni kwakuwa wenzetu walikuwa wamejaa nyuma wakijaribu kujilinda. Mabadiliko yaliyofanywa na kocha pia yakaongeza nguvu ndio maana tukaweza kuibuka na ushindi.”
Kipindi cha pili Lwandamina aliwatoa Hassan Hamisi Ramadhani ‘Kessy’, Saidi Juma Makapu na Obrey Chirwa na nafasi zao kuchukuliwa na Juma Abdul, Haruna Niyonzima na Matheo Anthony.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha jumla ya pointi 59 sawa na Simba wenye pointi 59 Yanga wanaongoza msimamo kwa tofauti ya magoli ya kushinda na kufungwa wakiwa wamebakiwa na michezo minne huku Simba akiwa na Mechi tatu na kesho atashuka uwanjani kucheza na African Lyon.

No comments