Header Ads

Responsive Ads Here

MSHAURI WA SOKA LA VIJANA MKONGWE ROGER MILLER AUMIZWA NA KIKOSI CHAKE CHA CAMEROON BAADA YA KUPOTEZA MCHEZO WA JANA


index
Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha EFM Bw. Maulid Kitenge kushoto akiwa na Mshauri wa soka la Vijana Cameroon na mchezaji wa Zamani wa timu ya taifa ya Cameroon Roger Miller kabla ya kuanza kwa mchezo katika Cameroon na Serengeti Boys.


Mshauri wa Soka la Vijana la Cameroon ambaye pia ni mchezaji Gwiji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Camroun  Roger Miller  ambaye ndio mchezaji aliyeishtua Afrika na dunia kwenye kombe la dunia  baada ya kuifungia timu yake dhidi ya Italia bao 1-0 katika fainali za kombe la dunia zilizofanyika Italia 1990 ameumizwa na kiwango cha timu yake kilichoonyeshwa leo katika mchezo na Serengeti Boys.
Gwiji huyo amesikitishwa na kiwango cha vijana wake mara baada ya kufungwa goli 1-0 mjini Yaunde leo akionekana kukerwa na kilichotokea baada ya kushauri mambo mbalimbali ya kiufundi katika timu hiyo ya vijana ya Cameroon ushauri ambao haukuzaa matunda katika mchezo wa leo mbele ya vijana wa kocha Bakari Shime kocha wa Serengeti Boys
Akizungumzia mchezo huo Kocha Bakari Shime amesema timu sasa imeiva watanzania wakubali kwamba Serengeti Boys Imeiva kwa michuano ya Gabon.
Ameongeza kwamba Jambo kubwa ni watanzania kuwa kitu kimoja kutuombea na kukubali kwamba sasa vijana wao wameiva kugombea nafasi ya kwanza kwa vijana katika michuano hiyo, amesifu vijana wake kwa kucheza kiwango kizuri na kutumia nguvu za kutosha kulinda goli lao.
Mfungaji wa gioli pekee la Serengeti Boys Ally King’azi amesema mchezo ulikuwa mzuri lakini anawashukuru wachezaji wenzake kwakuwa wote kwa ujumla wamefuata maelekezo ya mwalimu na ndiyo maana wakacheza vizuri.
Anasema toka mpira haujaanza mwalimu alimuelekeza mambo mengi ili kuhakikisha anapata goli na anashukuru maelekezo ya mwalimu yamemsaidia akishirikiana na wachezaji wenzake.
Ameongeza kwamba wanaenda Gabon ili kuhakikisha wanafika fainali na lazima iwezekane kwa sababu wameiva sasa japokuwa bado mambo kadha wa kadha lakini wanakwenda Gabon kupambana na wanawaza  kupata mafanikio na si vinginevyo.
Serengeti Boys inatarajiwa kucheza mchezo wa marudiano na timy ya Cameroon siku ya jumatano wiki ijayo kabla ya kuelekea nchini Gaboni kwa kambi ya wiki moja kabla ya kuanza kwa michuano ya AFCON U17 Mei 14/2017.

No comments