Header Ads

Responsive Ads Here

MKUU WA WILAYA YA MBOGWE AONGOZA ZOEZI LA USAFI WA MAZINGIRA.


mbo01
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mh Martha Mkupasi ameongoza wakazi  wa Mbogwe  kwenye Zoezi la Usafi wa Mazingira kwa kufanya usafi eneo la  Kituo cha Afya Masumbwe na maeneo yanayozunguka kituo hicho.

Akiongea  na wananchi baada ya zoezi la usafi, mh Mkupasi  amewataka wananchi kujijengea tabia ya kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguka kila siku na wasisubiri mwisho wa mwezi kwani kwa kupenda usafi  itawasaidia kujiepusha na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu. Pia amewasisitiza wananchi kutunza mazingira na kuepuka kukata miti ovyo badala yake wapande miti ya kutosha  .
Pamoja na hayo mh Mkupasi aliongea na Vijana wa  Kikundi cha Scout  walioungana na wananchi kwenye zoezi la usafi , nakuwahimiza kupenda masomo yao ya kila siku na kuweka bidii kwani bila elimu hawezi kutimiza ndoto zao .
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi  Mtendaji Wilaya, Afisa Mazingira wa Wilaya Charles Karibu Tuyi aliwashukuru wananchi na kikundi cha scouti kwa kujitolea kuja kufanya usafi wa mazingira kwenye kituo cha afya Masumbwe  na kuwahimiza kuendelea kusafisha mazingira wanayoishi na kuwataka waepuke kutupa uchafu kwenye mitaro kwani  utupaji wa taka ngumu unaweza kuziba mitaro na kusababisha  mafuriko .
mbo1

No comments