Header Ads

Responsive Ads Here

MKUU WA MKOA WA ARUSHA,MRISHO GAMBO AMPONGEZA MFUGAJI KWA KUWEKEZA KWENYE HOTELI


Askofu
wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini
Kati,Solomon Masangwa akizumza katika sherehe ya uzinduzi wa hoteli ya
Eseriani Kata ya Levolosi jijini Arusha na kumpongeza mmiliki kwa kufuga
kisasa na kuwekeza kwa kutoa ajira na kuongeza huduma bora kwa wageni
wanaofika Arusha.

Mkuu wa wilaya mstaafu,,Peter Toima akitoa salamu zake kwa wananchi walihudhuria.

Mkuu
wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza katika sherehe hiyo,kulia ni
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Arusha,Michael Lekule
Laizer.

Askofu
wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri
Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Solomon Masangwa akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa hoteli hiyo wanaoshuhudia kushoto ni 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha,Michael Lekule Laizer na Mkuu wa mkoa,Mrisho Gambo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizindua hoteli ya Eserian ,kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa
Arusha,Michael Lekule Laizer.

Mmiliki
wa hoteli ya Eserian,Issaya Yassi(kulia)akimweleza Mkuu wa mkoa,Mrisho
Gamb(wa pili kushoto),Askofu Masangwa(kushoto) na 
Mwenyekiti CCM mkoa wa
Arusha,Michael Lekule Laizer namna alivyotumia mifugo kuwekeza kwenye nyumba ya wageni.

Mkuu
wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akiangalia mandhari ya hoteli ya Eserian
akiwa na  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa
Arusha,Michael Lekule Laizer.

Mfanyabiashara
maarufu  wa jijini Arusha,Philemon Mollel maarufu kwa jina la
Monaban(kushoto)akikabidhiwa tuzo maalumu na Mkuu wa mkoa wa
Arusha,Mrisho Gambo iliyotolewa na shirika la kidini World Mission
International kwa kutambua mchango kwa jamii.

No comments