Header Ads

Responsive Ads Here

MD KAYOMBO ASHAURI WATANZANIA KUFUATA FURSA ZILIPO


Mkurugenzi wa
Manispaa ya ubungo Ndg John Lipesi Kayombo

Watanzania wametakiwa kuwa na utamaduni wa kuzifuata fursa zilizopo katika maeneo
mbalimbali nchini ili kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za
kukuza uchumi wa viwanda.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa
Manispaa ya ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akizungumza wakati
akitoa taarifa ya mbio za Mwenge unaotaraji kuzuru katika Manispaa ya
Ubungo Tarehe 31, Mei 2017.
Alisema kuwa katika mikoa mbalimbali Mwenge wa Uhuru ulipopita umekutana
na fursa ambazo Watanzania wakizitafuta na kuzifanyia kazi
wataondokana na uvivu, kukaa bila kufanya kazi na umasikini kwa kuwa
sasa Serikali iliyopo madarakani ni ya kazi.
Aliongeza kuwa, nchi
nyingi zimekuwa kiuchumi kupitia viwanda na kwa kuwa Serikali ya Awamu
ya Tano imedhamiria kukuza uchumi wa viwanda, wananchi wanapaswa
kuzichangamkia fursa mbalimbali ili kufanikisha dhamira ya Serikali
kufikia uchumi wa viwanda.
MD amesema kuwa Mwenge wa Uhuru katika
Manispaa ya Ubungo utapita katika Miradi mitano ya Maendeleo ambapo
Miradi minne kati ya hiyo itazinduliwa na Mradi mmoja wa Ujenzo wa Kituo
cha Polisi Gogoni utawekwa jiwe la Msingi.
Alisema kuwa Miradi
yote hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 itagharibu
jumla ya shilingi Bilioni 2,854,647,991.89
Imetolewa Na;
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

No comments