Header Ads

Responsive Ads Here

MAN UNITED MABINGWA KOMBE LA EUROPA LEAGUE,SASA KUSHIRIKI CHAMPIONS LEAGUE 2017-18


40C28C0F00000578-4539134-image-a-46_1495662259658
Manchester United wameshinda fainali ya Kombe la Europa kwa kuifunga Ajax Amsterdam kwa mabao 2-0 mjini Stockholm Sweden,Magoli ya Paul Pogba na Hendrick Mkhitaryan yameipa United sio tu Kombe bali pia nafasi ya kucheza Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.

40C1DF4500000578-0-image-a-79_1495656299309
Mapema kabla ya mchezo huo kuanza, timu hizo mbili zilitoa heshima zao kwa watu waliopoteza maisha katika shambulio mjini Manchester. Pia wachezaji wa Manchester United walivaa vitambaa vyeusi mikononi kama ishara ya heshima kwa waathirika.
Wakicheza bila ya mfungaji bora wao Zlatan Ibrahimovic, pamoja na mabeki Marcos Rojo, na Luke Shaw, pamoja na Erick Bailly anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu, kikosi cha Mourinho kililazimika kujituma kwenye mchezo huu wa 64 msimu huu.
40C0EAB900000578-4539134-image-a-25_1495661448117
Wakitumia uzoefu, pamoja na jinsi walivyojipanga, waliweza kukisumbua kikosi cha Ajax ambacho kilikuwa na wachezaji chipukizi, wakiwa na wastani wa umri wa miaka 22.
Manchester United sasa wanaungana na Chelsea, Tottenahm na Manchester City katika kucheza Klabu Bingwa Ulaya. Pia ushindi huu utawaingizia kitita cha takriban pauni milioni 50.
40C2929C00000578-4539134-image-a-56_1495662422666
Hili ni kombe la Pili Mourinho anashinda na United katika msimu wake wa kwanza. United walishinda Kombe la Ligi mwezi Februari.
40C2669500000578-4539134-image-m-78_1495662639506

No comments