Header Ads

Responsive Ads Here

MAKAMU WA PILI WA ZANZIBAR AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUTUMIA VIZURI KALAMU ZAO


img_2758
Na ALI Issa Maelezo-Znzibar
Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema wandishi wa habari  watumie vizuri kalamuzao na wanapo andika habari zao wazifanyie uchunguzi  kwa makini isiwe kukurupuka kuzitangaza kwani zinaweza kuwaletea matatizo wao wenyewe ua kusababisha matatizo makubwa kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Hayo ameyasema leo huko kilimani katika ukumbi wa chuo cha babari na masiliano katika maazimishi ya siku uhuru wa habari dunini.
Amsema Kumewahi kutokea matatizo mengi duniani yalio sababishwa na wandisha wa habari kwa kuitumia vibayo kalamu yao au kushabikia mambo bila utafiti jambo ambalo limesababisha maafa makubwa na kupelekea kupoteza roho za watu wasio nahatia katika mataifa yao.
Akitoa mfano wa baadhi ya taifa lilo kubwa na mkasa huo, alisema vita vya iraki nimoja ya mfano mmbaya ambao ulishabikiwa na wandishi wa habari kulazimisha iraki kumiliki silaha za sumu na kupelekea kuvamiwa kituambacho kilikuwa si kweli.
Amsema wandshi wajiepushe na masuala kama hayo kwani hilo nitatizo ambalo halite saulika katika historia ya binaadamu.
“Musishabikie tu kwa kuandika habari ambazo hamja zifanyia uchunguzi au mkatumiwa na watu kwamaslahi binafsi mtasababisha matatizo katika nchi au jammi husika ”alisema Balozi.
Aidha alisema kuwa serikali ya mapinduzi ya zanzbar ipo karibu sana na wandishi wa habari ndio maana hivi karibu Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk.Ali Muhamed Shein aliwaita wandishi wa habari kwa nyakati tafauti na kuwataka  watafute habari kwa viongazi wa serikali kila pale wanapo gundua kuna habari waende kudadisi.
Amsema mwandishi mzuri niyule anae tumia vyema kalamu yake naasie kubali kutumiwa na wana siasa,wafanya biasha na watu wengine kwa maslahiyao binafsi.
Aidha balozi alisema serikali ya Zanzibar inaheshimu uhuru wa habari na itaendelea kuulinda uhuruhuo kwani uhuru wa habari ndio unao leta utawala bora katika nchi na uwajibikaji kazini.
Hatahivyo aliwataka wandishi wa habari kundika habari za rushwa na madawa ya kulevya na kufichua maovu ya wale wanao tumia vibaya madaraka yao kwani ndio yanayo uimiza jamii na serikali.
Nae mwalimu mkuu wa chuo cha habari na mawasiliano DK Chande Omari alimshukuru kiongozi kwa maelekezo kwa wanahabari na kusema maelekezo hayo watayafanyia kazi.
Aidha kiongozi huyo aliishukuru Serikali ya Zanzibar kwa kuwajengea chuo kinacho endana na taaluma zao kitu ambcho wanatoa wanafunzi waledi wa fani ya habari.
Amesema hali hiyo ni yakupongeza lakini isishiehapo bali serikali iendelee kuwapa msukumo kwa kuwapatia vifaa vya kusomeshea ili watoe wanafuzi waledi zaidi.
Sherehe hizo ziliambatana na ngoma na mashairi yenye ujumbe wa mwaka huu umakini wafkra kwa nyakati ni muhimu.

No comments