Header Ads

Responsive Ads Here

MAELFU WATOA HESHIMA ZAO ZA MWISHO KWA WALIOFARIKI KATIKA AJALI MKOANI ARUSHA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, ameungana na maelfu ya Watanzania kushiriki ibada ya kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent ya mkoani Arusha, waliofariki katika ajali ya basi dogo juzi Mei 06,2017 wakielekea kwenye ziara ya kimasomo ya ujirani mwema, katika eneo la Karatu.

Wakati huo huo bunge la Tanzania limeungana na waombolezaji wengine kwa kuahidi kutoa posho ya siku moja kama rambirambi kwa familia zilizofikwa na msiba huo.

mtandao wa www.habari za jamii.com tunatoa pole kwa wote walioguswa na msiba huu mzito. #TaifaLinaomboleza #DaimaTutawakumbuka
Taswira ya waombolezaji,  uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.#PichaNaMitandaoMbalimbali

No comments