Header Ads

Responsive Ads Here

LUKUVI AMPA SIKU SABA MBUNGE KULIPA KODI YA ARDHI


index
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amemtaka mbunge wa kwimba Mhe. Shannif Mansuri alipe kiasi cha shilingi million 529 ambayo ni malimbikizo ya Kodi ya pango la ardhi  tangu mwaka 2010 ndani ya siku saba.
Waziri Lukuvi amesema hayo alipokuwa katika ziara yake Mkoani Mwanza wilaya ya Nyamagana na kufanya ukaguzi katika mfumo wa kodi ambapo aligundua watu wenye madeni makubwa ya pango la ardhi akiwemo mbunge huyo.

Baadae ya kugundua hilo ikamlazimu kutoa agizo kwa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la wilayani Nyamagana kuhakikisha mbunge huyo analipa deni hilo ndani ya siku saba kinyume na hapo ni kupigwa mnada eneo lake au kufutiwa hati yake.
Aidha, katika ukaguzi huo pia aligundua urasimu na uzembe wa watendaji wa jiji la Mwanza katika sekta ya ardhi, ambapo ameona kwenye baadhi ya mafaili kuwepo kwa watu wanaofuatilia hati zao zaidi ya miaka mitano bila mafanikio. Hivyo, Waziri Lukuvi alichukua hatua za kupiga simu kwa mmoja wa watu hao ili kuthibitisha ni kwa nini hajapewa hati ambapo aligundua kuwa amekuwa akizungushwa na watumishi hao. Hapo alitoa agizo kwa watendaji hao kutoa hati kwa Mama huyo na wengine wote haraka iwezekanavyo.
Mh. Lukuvi amewaeleza watendaji wa jiji la Mwanza mbele ya Mkuu wa Mkoa John Mongella kufuatilia kwa karibu mfumo wa kodi ya pango la ardhi, na utoaji wa hati kwa wananchi kwa kuwa masuala hayo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa, sababu huongeza pato la serikali hivyo kuinua uchumi wa nchi.

No comments