Header Ads

Responsive Ads Here

KUTOKA SHAHIRI HADI KUWA KINYWAJI CHA BALIMI EXTRA LARGER


BALIMI

BALIMI2
wakulima mbalimbali wakionyesha mashamba ya shahiri mkoani Arusha
BALIMI3BALIMI4BALIMI5
Shahiri ni moja ya malighafi muhimu katika kutengeneza bia
 
…………………..
Uzalishaji wake unakuza uchumi na kuleta maendeleo endelevu kwa jamii
Safari yenye historia ya kuvutia ya zao la Shahiri hadi kuwa kinywaji cha bia ya Balimi Extra Lager inaanzia mbali na eneo la Usukumani ambako ndipo asili ya bia hii ambayo  zaidi ya kuwa kinywaji cha kukataa kiu inachangia kuongeza pato la serikali kubadilisha maisha ya jamii kuwa bora.
Bia ya Balimi inatengenezwa na kampuni ya TBL Group,iliyopo chini ya kampuni ya kimataifa ya ABin Bev.Inatengenezwa kwa kutumia malighafi zilizozalishwa nchini Tanzania ambapo  inachangia pato la serikali na kuchochea maendeleo endelevu kwenye jamii.
Katika wilaya ya Hanang mkoani Manyara na kwenye mikoa ya Kilimanjaro,Arusha na Njombe wakulima wanapanda mbegu moja moja ambazo zinawezesha kupatikana mavuno mazuri ya Shahiri inayotumika kutengeneza bia ya Balimi kwa ubora ikiwa na ladha ya aina yake inayovutia .
Wakulima ni wawezeshaji wakuu wa kufanikisha mchakato wa nchi yetu  kuelekea katika uchumi wa viwanda.TBL Group ikiwa inaendesha viwanda vikubwa vya kutengeneza pombe nchini ni moja ya mdau mkuu wa  kuendeleza sekta ya viwanda ikiwa inafuata  mwongozo  unaojulikana kama ‘’Dunia Maridhawa ‘’kufanikisha suala hili.
Chini ya mwongozo huu wa ‘Dunia Maridhawa’ itaweza kubadilisha maisha kwa kila mdau anayechangia kufanikisha utengenezaji wa bia  ya Balimi na bia  za chapa nyingine zinazotengenezwa na TBL Group zilizopo kwenye masoko.
TBL Group imekuwa ikishirikiana na wakulima kwa kuwafundisha mbinu bora za kilimo cha kisasa kuwezesha kupata mavuno zaidi,pia imekuwa ikiwaunganisha na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa kuwawezesha kuuza mazao yao ya ziada kwa bei nzuri pia imekuwa ikiwaunganisha na mabenki na taasisi nyingine za kifedha kwa ajili ya kupata mikopo nafuu na huduma nyinginezo za kifedha.
Kupitia ushirikiano huu maisha ya wakulima zaidi ya 30,000 yamebadilika na kuwa bora zaidi kutokana na shughuli zao za kilimo ambapo wameweza kuuza malighafi ya kutengenezea Balimi na bia nyinginezo zinazotengenezwa na TBL Group  na kupata faida na kuweza kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kujenga mashule,vituo vya afya,kupata maji safi na kufanya mambo mengineyo mengi ya maendeleo.
Uzalishaji wa bia ya Balimi na nyinginezo mbali na kuchangia pato la Taifa kwa njia ya kulipa na kukusanya kodi za serikali pia umewezesha jamii kunufaika kutokana na miradi mbalimbali inayotekelezwa na TBL Group kuanzia miradi ya kusaidia elimu,kusambaza maji safi kwa jamii,kampeni za usalama barabarani,na miradi ya afya.
Uhusiano na ushirikiano wa TBL Group  na wakulima mbali na kuwanufaisha kampuni na wakulima unanufaisha    mzunguko wa wadau wetu mbalimbali katika biashara za kampuni wakiwemo viwanda vya kutengeneza chupa ,wasambazaji wa bia, mlolongo huu wa wanufaikaji unaenda mpaka kwa watumiaji wa kinywaji cha bia baridi ya Balimi Extra Lager.
Jina Balimi lina maana ya mkulima kwa lugha ya  Kisukuma moja ya kabila kubwa katika kanda ya ziwa Victoria ambalo linakishughulisha na Kilimo na Ufugaji.Kutokana na uhalisia wa mila za kabila hili na maisha yao ya kila siku,bia ya Balimi imebuniwa kuelezea maisha ya jamii yenye asili ya jina lake na utamaduni wao.
Balimi ni bia yenye ladha nzuri na ya kipekee na imetengenezwa kwa maji asili kutoka ziwa Victoria.Chupa yake nzuri ambayo inaifanya kuwa na mwonekano wa rangi ya jua linalozama unatoa taswira ya hali halisi ilivyo na watu wanaoishi katika eneo inakotengenezwa.Balimi inatangazwa uzuri asilia wa maeneo ya kanda ya ziwa Victoria na utamaduni wa kabila la Wasukuma

No comments