Header Ads

Responsive Ads Here

KINANA AKUTANA NA BALOZI WA JAMHURI YA KOREA KUSINI HAPA NCHINI.


KORE1
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg Abdulrahman Kinana akutana na Balozi wa Jamhuri ya Korea kusini hapa nchini Mhe Song Geum-Young alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es salaam, leo Mei 29, 2017.

Katika mazungumzo yao, wamehimiza suala la kuboresha mahusiano baina ya Jamhuri ya Korea Kusini na Tanzania pamoja na kuzungumzia ushirikiano wa muda mrefu katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.
KORE2
KINN
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akihojiwa na Mwanishi wa Kituo cha Televisheni cha China Central Television – CCTV kuhusu mafanikio ya kiuchumi ambayo China imeyafikia na hatua mbalimbali za maendeleo ambazo Tanzania inajifunza na kushirikiana na China ili kufanikiwa kufikia uchumi wa kati.

No comments