Header Ads

Responsive Ads Here

Kilimanjaro Lager yaingia ‘Beer for Africa’


KILI
-Kuuzwa pamoja na chapa maarufu 8 za Afrika duniani kote
-Kuchangia kuondoa changamoto ya lishe kwa wanafunzi  barani Afrika
 
 Bia ya Kilimanjaro inayotengenezwa na kampuni ya TBL Group chini ya kampuni mama ya  kimataifa ya ABInBev imejumuishwa pamoja na bia zingine vinara kutoka nchi mbalimbali  8 za Afrika na kutangazwa kuwa ‘Beers for Africa’ ambapo zitauzwa sehemu mbalimbali duniani  zikiwa katika kifungashio cha boksi kimoja.
 
Mpango huu wa kuunganisha chapa maarufu za Afrika kusambazwa kwa pamoja umezinduliwa nchini Afrika ya Kusini  na baadaye bia hizo 8 za kopo zilizopo kwenye kifungashio kimoja cha boksi zitasambazwa katika masoko nje ya bara la afrika  lengo kubwa likiwa ni kukuza masoko ya chapa hizo  katika ngazi ya kimataifa.
 
Chapa za bia ambazo zimechomoza na kuingizwa kwenye mpango huu ni Kilimanjaro Lager (Tanzania),Castle Lager (Afrika ya Kusini),St.Louis (Botswana),Maluti Premier Lager (Lesotho),2M,Laurentina na Manica (Msumbiji)  na Zambezi Premier Lager (Zimbabwe).
 
“Tunajivunia  bia yetu ya Kilimanjaro kuingizwa katika chapa za Afrika zitakazosambazwa kwa pamoja duniani na hatua hii inadhihirisha dhamira yetu kuu ya kuwaleta watu wote pamoja katika dunia maridhawa”Imeeleza taarifa ya kampuni ya TBL Group iliyotelewa jijini Dar es Salaam .
Mbali na kusambazwa  kwa  pamoja na chapa nyingine bia ya Kilimanjaro imeingizwa  katika mpango wa kuboresha lishe barani Afrika kwa ushirikiano na na  Shirika lisilo la Kiserikali la Stop Hunger Now.
 
Kupitia mpango huu boksi la chapa za bia za Afrika sehemu ya fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo yake zitasaidia kuwapatia chakula chenye lishe wanafunzi wapatao milioni 1 hadi kufikia mwaka 2018.
 
“Tunajivunia ndoto yetu ya kusaidia kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye jamii kupitia mpango huu wa Beers for Afrika kukabiliana na tatizo la utapiamlo lililokithiri katika ukanda wa Afrika”.Imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

No comments