Header Ads

Responsive Ads Here

KENNY ALLY ATUA SINGIDA UNITED NA KUZITOZA YANGA ,AZAM FC


IMG-20170525-WA0016[1]
Matajiri wa Mkoa wa Singida ambao wamepanda Ligi Kuu Msimu huu wameanza kujiweka fiti katika usajili wa wachezaji wa ndani na mchezaji wa kwanza kusaini ni Kiungo Mkabaji wa Mbeya City, Kenny Ally MWambungu sasa ni mali ya Singida United.

Huu ni usajiri wa sita baada ya kuwasajili wachezaji watano wa kigeni na kwa mujibu wa katibu Mkuu wa klabu hiyo inataka kusajili jumla ya wachezaji 14.

Kenny Ally alikuwa kwenye vichwa vya habari katika timu kubwa zilizokuwa zinawaania saini ya mchezaji huyu wakiwemo wakongwe Simba na Yanga na nyingine kama vile Azam FC,Mwadui Fc.
Singida United ambayo ipo chini ya Kocha mwenye mafanikio Tanzania hata bara la Afrika na mwenye uzoefu wa Ligi Hans Van Der Pluijm ambaye alikuwa kocha wa Zamani wa Mabingwa wa Kihistoria Yanga ambapo aliwapa mataji mawili mfululizo hata huu ubingwa wa tatu unachangizwa na Juhudi zake kwani aliiongoza Msimu wa kwanza na msimu wa pili alimuachia George Lwandamina

No comments