Header Ads

Responsive Ads Here

KATIBU WA CCM MKOA WA ARUSHA AKUMBUSHA WAJIBU WA WATUMISHI


unnamed
Katibu wa ccm Mkoa wa Arusha Ndg. Ernest Mpanda (aliyesimama) akizungumza na watumishi wa Jiji la Arusha (hawapo pichani) katika Kikao Maalumu alichoitisha kuzungumza na watumishi hao.

1
Katibu wa Ccm Wilaya ya Arusha Ndg. Ramadhani Dalo akiteta jambo na Katibu Mwenezi wa Ccm Mkoa wa Arusha Ndg. Shabani Mdoe wakati wa Kikao na watumishi wa Jiji la Arusha.
2
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro(aliyesimama) akizungumza na watumishi wa Jiji wakati wa Kikao
3
Afisa Usafishaji wa Jiji la Arusha Ndg. James Lobikoki (aliyesimama) akiuliza swali kwa Katibu wa Ccm Mkoa wa Arusha wakati wa Kikao.
4
Mtumishi wa Jiji Ndg. Privcanus Katinhila akiuliza swali wakati wa Kikao na Katibu wa Ccm Mkoa.
…………………………

Nteghenjwa Hosseah
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ndg. Ernest Mpanda amekutana na
watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ambapo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wajibu wao katika Utumishi wa Umma kwa kusimamia maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Amesema kuwa watumishi wote walioajiriwa na Serikali hii ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais Dr. John Joseph Pombe Magufuli yawapasa kutekeleza yale yote yaliyoainishwa kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi na si vinginevyo.
Haiwezekani Mshahara ulipwe na Serikali ya Ccm alafu utakeleze kazi za upande mwingine, hilo siwezi kulivumilia kama unaona huwez kutenda yale tunayotaka sisi wenye Ilani ni bora ukatupisha ili nafasi hiyo ichjukuliwe na wengine wenye moyo wa kuijenga Nchi yao alisema Mpanda.
Aliongeza kuwa Serikali ya Ccm inatambua na kutahmini kazi kubwa mnayoifanya na ndio maana tuko nanyi bega kwa bega kuhakikisha kwamba tunapata matokea Chanya lakini kwa wale wachache watakaotuangusha hatuna huruma nao watawashughulikia ipasavyo.
Katika mfululizo wa vikao vyake ambapo ameanza kuzungumza na watumishi wa Makao Makuu ya Jiji na ataendelea katika maeneo mengine ya Jiji amewataka watumishi kufanya kazi kwa uadilifu huku wakisimamia mali za uma kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqqaro
amewataka watumishi wa hao wa Jiji kutumikia Umma wa kwa kadiri ya taaluma zao na weledi wa hali ya juu.
Kazi hizi mlizitafuta wenyewe na unafahamu majukumu yale yaliyopelekea wewe kuomba kazi hii sasa ukishaipata ndio unatakiwa kuonyesha uwezo wako katika utendaji ili basi wananchi hawa ambao wewe unalipwa kwa kodi zao waweze kuhudumiwa ipasavyo.
Mnatakiwa mzingatie miongozo ya Utoaji wa hduma bora na mhakikishe mnatumia Lugha nzuri, ukarimu na usikivu wa shida za wananchi ili tupunguze malalamiko katika ngazi za Juu alisema Daqarro.

No comments