Header Ads

Responsive Ads Here

‘KABURU’ YANGA WANASHANGILIA UBINGWA HEWA,SIMBA INA NAFASI YA KUTWAA UBINGWA VPL


unnamed
Simba wanatakiwa kushinda zaidi ya mabao nane katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu huku wakiomba Yanga ipoteza kwa zaidi ya mabao matano dhidi ya Mbao FC mjini Mwanza ili wao wawe mabingwa.
Lakini hiyo haiwakatishi Simba tamaa na hawataki kusikia Yanga wakitangazwa kuwa mabingwa kabla ya mechi yao ya mwisho wao wakiwavaa Mwadui FC jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesisitiza bado wanataka kuona matokeo hadi mechi ya mwisho.

“Sisi tunajua bingwa bado hajapatikana na tutaona hadi katika mechi ya mwisho. Tutapambana hadi tone la mwisho.

“Hatuwezi kukata tamaa, huu ni mpira na vijana wako vizuri kabisa,” alisema akionyesha kujiamini.
Endapo mechi ya mwisho Yanga atakubali kufungwa atakuwa na pointi 68 sawa na Simba ambao viongozi bado wanaamini kuwa pointi tatu walizopokonywa dhidi ya Kagera Sugar zitarudishwa kwani wanataka kwenda FIFA kudai pointi zao na watakuwa na pointi 71.

No comments