Header Ads

Responsive Ads Here

JUMIA TRAVEL YAWALETEA ' TRAVEL SMART' WATEJA WAKE WAAMINIFU

 Na Jumia Travel

Katika jitihada za kurahisisha huduma za hoteli na usafiri, Jumia Travel imekuja na programu mpya ya ‘travel smart’ kwa wateja wake waaminifu nchini Tanzania. Programu hii imelenga kuwaongezea thamani wateja kwenye huduma watakazozitumia ikiwemo punguzo maalumu kuanzia 10% mpaka 20% pamoja na ofa mbalimbali za ndege na vifurushi vya likizo. Pia inakuja na vitu vya ziada kama vile kuchelewa kutoka, usafiri wa bure kutokea uwanja wa ndege, kukaribishwa na kinywaji cha bure pamoja na kuwahi kuingia hotelini tofauti na wateja wengine wa kawaida.


Akizungumzia juu ya huduma hiyo mpya kwenye mtandao wa kampuni hiyo, Meneja Mkaazi kwa hapa Tanzaia, Bi. Fatema Dharsee amesema kwamba dhumuni kubwa ni kuonyesha kuwajali na kuwazawadia wateja wao waaminifu wanaotumia huduma zao mara kwa mara kwa ajili ya malazi au kukata tiketi za ndege.

“Lengo kubwa la Jumia Travel ni kuhakikisha kuwa tunawezesha huduma za malazi na usafiri ndani na nje ya Afrika kuwa rahisi na nafuu. Kwani tunaamini kwamba licha ya gharama ambazo mteja atazitumia lakini bado anastahili ubora wa hali ya juu na uzoefu wa kipekee. Kwa kufanya hivyo itamfanya aendelee kutumia huduma zetu zaidi na hata kuwashawishi watu wake wa karibu kufanya hivyo pia,” alisema Bi. Dharsee.

“Kupitia programu hii mpya tuliyoizindua, inamaanisha kwamba sasa wateja ambao wamekuwa wakitumia mtandao wetu kupata huduma za malazi na usafiri wa ndege mara kwa mara watapatiwa ofa za punguzo la bei ambalo wateja wengine hawawezi kuzipata wala kuziona. Wateja wengine wa kawaida watakaokuwa wanatembelea mtandao wetu wataona bei za kawaida na sio za ‘travel smart’ Ili kunufuaika na huduma hii mpya lazima mteja awe amejisajili au kuwa na akaunti kwenye mtandao wa travel.jumia.com ndipo ataweza kuziona ofa hizo kutoka kwa hoteli mbalimbali tulizoingia nazo makubaliano,” alihitimisha Meneja Mkaazi wa Jumia Travel nchini.


Programu hii mpya ya ‘travel smart’ kutoka kwa Jumia Travel pia itakuwa na manufaa makubwa kwa hoteli washirika kwani itawawezesha kuona idadi ya wateja waliosajiliwa na huduma hii kwani wao pekee ndio wanaweza kuzifaidi ofa hizi. Hii itazisaidia hoteli zao kuonekana au kutangazwa zaidi na kuwaongezea masoko kupitia kampeni maalum inayofanyika kuitangaza miongoni mwa wateja.

No comments