Header Ads

Responsive Ads Here

JICA Yaipongeza Muhimbili Kwa Kuboresha Huduma


unnamed
Mkurugenzi  wa  Utumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Makwaia Makani akitoa neno kwa wauguzi wa  Hospitali hiyo katika mkutano wa kupokea mrejesho kuhusu mpango wa kuboresha huduma na kutatua matatizo madogo  kwa kutumia rasilimali zilizopo-KAIZEN .

A
Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimsikiliza Mkurugenzi wa Utumishi wa MNH  Bwana: Makani katika  mkutano huo uliofanyika  jana.
Bi Rose  Mpayo  Muwezeshaji kutoka Hospitali ya  Rufaa Kanda ya Mbeya akielezea umuhimu wa utoaji huduma bora kwa wateja.
004: Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia maelezo kutoa kwa mtoa mada.
005: Mtaalam wa usimamizi wa huduma  bora kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan- JICA  -Noriyuki  Miyamoto akitoa mrejesho kuhusu  mpango wa kuboresha huduma . Zoezi lililofanywa na JAICA kwa kushirikiana na  wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto  kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan –JAICA- wametoa mrejesho wa utekelezaji wa mpango wa kuboresha huduma na kutatua matatizo madogo kwa kutumia rasimilimali zilizopo –KAIZEN.
Mbali na kutoa mrejesho huo pia wameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuboresha utoaji wa huduma.
Mpango huo ambao unahusisha watoa huduma umesaidia watumishi kutoa huduma bora,  kuzingatia muda wa utoaji huduma na hivyo kupunguza malalamiko kwa wateja.
‘’ Tumefanya tathimini tumeona jinsi ambavyo mmeboresha utoaji wa huduma na kupunguza mlalamiko kwa wananchi , wauguzi wanahudumia wagonjwa kwa upendo na wanatumia lugha nzuri lakini hata mazingira ya Hospitali ni safi’’ amesema Noriyuki  Miyamoto.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utumishi wa MNH Bwana Makwaia Makani amesema tangu kuanza kutekelezwa kwa mpango huo mwaka 2008 kumekua na mabadiliko mengi hospitalini hapo na kusisitiza kuwa hospitali hiyo itahakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma bora.

No comments