Header Ads

Responsive Ads Here

Hamasika na Masika ya Mobisol yaibua washindi wengine


MOB1
Mwakilishi wa  kampuni ya umeme wa jua ya Mobisol wa mkoa wa Dar es Salaam,Allan Rwechungura (kulia) akiongea kwa simu na mmoja wa washindi wa droo ya promoshenu ya Hamasika na Masika inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo wateja wateja watatu walijishindia fedha taslimu na vifaa vinavyotumia umeme wa nishati ya jua (Kushoto )ni Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya taifa,Emanuel Ndaki .Droo hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

MOB2
Baadhi ya vifaa vya nishati ya jua vinavyosambazwa na Mobisol
…………………………………………………………………………….
 Kampuni ya Kijerumani ya Mobisol Tanzania inayosambaza nishati ya umeme wa jua na vifaa imara na vya kisasa vinavyotumia nishati hiyo nchini imefanya droo ya pili ya   kampeni maalumu ya kuhamasisha wananchi  kujiunga na mtandao wake inayojulikana kama “Hamasika na Masika”iliyozinduliwa mwezi Machi  ambapo washindi watatu wamepatikana na kujishindia zawadi mbalimbali.Mshindi wa kwanza katika droo hiyo ya pili iliyofanyika chini ya usimamiazi wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha  ni Bashiru Ijenge mkazi wa Kondoa,mkoani Dodoma aliyejishindia kitita cha shilingi 350,000/-mshindi wa pili ni Simon Peter Barbaid wa mjini Moshi aliyejishindia redio ya Mobisol stereo na mshindi wa tatu, ni Anna S Magulu,  mkazi wa Kikatiti, Arusha  aliyejishindia Jiko koa.

Kupitia kampeni hii wateja watakaonunua mitambo ya umeme wa nishati ya jua katika kipindi cha mwezi huu wa  Mei wataingia kwenye droo na kuweza kujishindia pikipiki aina ya Boxer na pia zaidi ya shilingi milioni 4 zimetengwa wa ajili ya kutoa zawadi za fedha taslimu kwa washindi ambapo pia wateja wa sasa wa Mobisol watakaoshawishi  wateja wapya kujiunga na mtandao wa Mobisol nao watashirikikishwa katika kampeni hii.

Mwakilishi wa Mobisol wa mkoa wa Dar es Salaam,Allan Rwechungura  anasema “Tunataka wateja wetu waweze kunufaika zaidi katika kipindi hiki kwa kuweza kujishindia zawadi mbalimbali pale wanaponunua mtambo wao wa Mobisol. Ni utamaduni wetu kugawana sehemu ya faida yetu na wateja wanaoifanya Mobisol kuwa kampuni bora ya sola katika ukanda wa Afrika mashariki”
Rwechungura alisema Shindano hili linawajumuisha wakazi wote wa mikoa zaidi ya ishirini Tanzania bara ambapo Mobisol inatoa huduma zake na kuitaja mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Kagera, Simiyu, Geita, Kigoma, Rukwa, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe,  Pwani pamoja na Morogoro.

Aliongeza kusema kuwa  kampuni ya Mobisol inauza na kufunga, mitambo ya bora ya Sola nchini pamoja na vifaa  vya matumizi ya nishati hii ambavyo ni  Paneli ya Sola, betri, taa, Televisheni, Radio, Tochi, Mashine ya Kunyolea nywele, MobiCharger (Kifaa cha kuchajia Simu) na Friji.

“Wakati ni huu kwa watanzania kupata nishati bora ya umeme wa jua na vifaa vya kisasa na natoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hii  kujiunga na  familia ya Mobisol waweze kuishi maisha ya kisasa na kujishindia zawadi kupitia kampeni hii ya ‘Hamasika na Masika’.Kwa maelezo zaidi ya kupata huduma za Mobisol mteja anaweza kupiga simu namba 0800 755 000 bure na utahudumiwa”Alisema.

Akiongea kwa niaba ya washindi,Bashiru Ijenge,ambaye ni mkazi wa Kondoa alisema kuwa wamefurahishwa na mkakati wa Mobisol wa kuwasogezea huduma za umeme wa jua  na vifaa bora ,imara na vya kisasa “Mobisol ni suluhisho la tatizp la nishati ya umeme hususani katika maeneo ambayo hayajapata umeme wa gridi ya taifa na umeme wao ni wa uhakika na vifaa wanavyosambazwa ni vya ubora wa hali ya juu vilivyotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu nchini Ujerumani”.Alisema.

No comments