Header Ads

Responsive Ads Here

Gihon Needy Comfort Organization kushirikiana na wadau kuleta maendeleo kwa jamii


wananchi
Taasisi isiyo ya kiserikali ya GIHON NEEDY  COMFORT  Organization imedhamiria  kushirikisha jamii wahisani wadau na maendeleo ikwemo serikali katika kupigania ustawi wa kuchumi kijamii na kiutamaduni ili kuondoa umaskini unyanyasaji na uonevu ili kuleta maendeleo.
 
Mkurugenzi mtendaji wa   GIHON NEEDY COMFORY  Organization bi REBECA STANFORD  amesema shirika hilo si la kisiasa limeundwa kwa nia ya kuhudumia na kusaidia jamii.
 
Shirika hilo imesasjiliwa chini ya sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali namba 24 ya mwaka 2002 na kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005 namba ya usajili  00NGo/08289 malengo ya msingi yashirika hilo ni kuwezesha wanajamii kiuchumi, kieleimu, kiafya nk.
 
Kwa kutambua michango mbalimbali ambayo imekwisha tolewa na mashirika mbalimbali ya maendeleo ya jamii hii iliyopopembezoni shirika la Gihon Needy Comfort Organization wako tayari kushirikiana kutetea haki za binadamu na kutoa Elimu pamoja na uchunguzi wa ufumbuzi wa matatizo ya jamii Inayowazunguka.
 
Bi REBECA STANFORDY ambaye ni mkurugenzi wa shirika hilo amesema shirika hilo limekuwa likifanya kampeni za uelimishaji kwa jamii kwa njia ya makongamano mikutano ,warsha na semina ili jamii iwatambue kuwapenda na kuwatathimini pamoja na kujitoa kwa hali na mali ili kusaidia kupambana na changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo kutoa elimu ya ujasiliamali sheria na elimu ya afya kwa husika ili kutimiza ndoto ya maisha bora kwa kila mtanzania.
 
Asasi hiyo inasimamia sheria na sera zinazotetea haki za Wajane, Yatima na wanaoishi katika Mazingira Magumu Tanzania na Afrika ili kurejesha matumaini mapya kwa jamii husika.
 
Bi REBECCA STANFORD ameendelea kusema kuwa shirika la GIHON NEEDY COMFORT Organization limekuwa likitoa misaada mbalimbali ya Vyakula, Mavazi, Makazi, na Mahitaji kwa wanawake Wajane, Wazee, na wenye maisha duni na kutoa ushauri nasaha Afya ya Uzazi.
 
Shirika hilo limekuwa likiungaunisha jamii ya Watanzania kuungana dhidi ya kampeni ya za VVU/UKIMWI kuwezesha utambuaji kwa watu wanaoishi ya Ukimwi.
 
Aidha shirika limekuwa likijihusisha na utunzaji  walengwa wake kwa kuwatembelea Majumbani kuwafariji na kuwapatia misaada ya hali na mali bila ubaguzi wa Imani, Rangi jinsia na kuhakikisha watoto Yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi wanajikomboa Kieleimu, Kiuchumi,na hata Kisheria.
 
Kila kukicha wapo Wajane, Wagane na Yatima wapya wanaotokana na vifo visivyotarajiwa kwa sababu mbalimbali na wapo watu wanaozaliwa na Ulemavu na wengine kwa sababu ya ajali za Barabarani na Majanga mbalimbali wapo wanaoishi katika katika Mazingira magumu na Watoto wa Kike wanaoathirika na Mimba za Utotoni lakini pia yapo majanga mbalimbali yanayoacha watu katika hali ngumu zaidi.
 
Hata hivyo bi REBECA ameongeza kuwa yapo mahitaji mbalimbali yanayo ikabili jamii ikiwemo ugumu wa maisha matibabu kwa wagonjwa mahitaji ya biashara,wajane kusomesha watoto na wengine kukosa chakula.

No comments