Header Ads

Responsive Ads Here

FAINALI ZA AFCON U-17 KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO NCHINI GABON


Ghana-u20
Fainali za Michuano ya 12 ya  Kombe la Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 zinatarajiwa kuanza leo mjini Franceville, Gabon hadi Mei 28, mwaka huu itakapofikia tamati.Mechi mbili za Kundi A zinatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Franceville kuanzia Saa 10:00 jioni kati ya wenyeji Gabon dhidi ya Guinea na baadaye Saa 1:00 usiku kati ya Cameroon na Ghana.

Mechi za Kundi B zitaanza kesho, kwa michezo miwili pia kuchezwa Uwanja wa Port-Gentil, ya kwanza Saa 9:00 Alasiri kati ya mabingwa watetezi, Mali na Tanzania wanaoshiriki kwa mara ya kwanza kabisa michuano hiyo na wa pili utazikutanisha Angola na Niger kuanzian Saa 12:00 jioni.

No comments