Header Ads

Responsive Ads Here

CHAMA CHA WAONGOZA WATALII TANZANIA (TTGA) WALIA NA MIUNDO MBINU MIBAYA YA BARABARA NDANI YA HIFADHI


Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa chama cha waongoza Watalii
Halifa Msangi,Wakwanza kushoto ni Katibu wa umoja huo Emanuel
Mollel,Haji Mbuguni Mjumbe wa (TTGA)Omari Rajabu mjumbe,Apolinary
Kiwhili M/Msaidizi wakiwa katika maonyesho ya utalii ya 18 ya 
Karibu
Wa
pili kulia ni mwenyekiti wa Chama cha  waongoza Utalii Nchinni
Tanzania Halifa Msangi,Wa kwanza kushoto Katibu wa chma hicho Emanuel
Mollel,wakiwa na wajumbe wa chama hicho ,pamoja na Hosiana F.
Siao.Picha na Vero Ignatus Blog.
Wakizungumza na wageni mbalimbali Ambao walitembelea
banda lao katika maonyesho ya Utalii yaliyo shirikisha zaidi ya
makampuni  300 ya utalii,amabapo washiriki wa ndani yanchi ni 60%
na yale ya nje ni 40% ambapo huwa wanafanyika lila mwishoni mwa mwezi
mei .Picha na Vero Ignatus Blog.
Chama cha waongoza Watalii wakiwa kwenye banda lao
ndani ya viwanja vya magereza katika maonyesho ya Karibu Fair yaliyo
beba kauli mbiu isemayao Utalii endelevu kwa Maendeleo.Picha na Vero
Iganatus Blog.
Maongezi yakiendelea na wageni waliotembelea banda
lao.Picha na Vero Ignatus Blog.
 
 
Chama cha waongoza Watalii nchini Tanzania
(TTGA) wameiomba Serikali iwapatie eneo huru kati ya Hifadhi  ya
Ngorongoro na ile ya  Serengeti ,kwani katika eneo hilo la Ndutu
katika upande wa Serengeti hakuna barabara za kufanyia mizunguko za
kwenda kuangalia wanyama .
 
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho ndugu Halifa Msangi
kwamba  changamoto kubwa wanayoipata kama waongoza watalii ,ni
kipindi ambacho wanyama pundamilia na Nyumbu wanapohama  kuelekea
upande mwingine hawawezi kuwapeleka wageni kwenda kuwaona wanyama hao
upande wa pili
“Katika
eneo la Ndutu wananyama pundamilia na nyumbu huwa wanatabia ya kuhama
na kuelemea  upande mwingine,sasa unakuta wewe muongozaji ukiwa
na kibali cha upande mmoja tu  huwezi kuwapeleke wageni mahali
wanyama walipo kwani hakuna barabara ya kufanyia mizunguko kwenda
kuwaona wanyama jambo ambalo tumekuwa tukipata changamoto kubwa na
maswali mengi kutoka kwa wageni tumeizungumzia changamoto hii kwa muda
mrefu sasa.”alisema Halifa.
Kwa
upande wake Katibu wa chama hicho cha waongoza watalii Emanuel Alfayo
Mollel amesema kuwa changamoto nyingine kubwa ni barabara zilizopo
ndani ya Hifadhi haswa kutoka Ngorongoro kuelekea Serengeti ,barabara
hizo zimejazwa vifusi kwa ya km 10 ambavyo havijasambazwa jambo ambalo
wakati mwingine vinaweza vikapelekea hata kusababisha ajali pale
ambapo dereva anahangaika kuvikwepa.
”jamani
miundo mbinu ndani ya hifadhi  haswa  Tarangire na Manyara
ni changamoto kubwa wakati wa mvua hakupitiki, “alisema
Emanuel.Amesema
kuwa asilimia 90 ya waongoza Watalii ni waajiriwa kwenye makampuni ya
Utalii ,hadi sasa mikataba yao imekuwa ni donda ndugu kwani mikataba
hiyi ipo tayari lakini hakuna wakuisimamia ili ifanye kazi kama
inavyohitajika.
Amesema  Waongoza watalii nchini Tanzania
kilianzishwa mwaka 1999,kina jumla ya wanachama zaidi ya 3000
,Wanachama ni 1130 ,wanachama hai waliolipa ada zao kwa mwaka 2017 ni
567 tu,amewataka waongozaji watalii hao ambao sio wanachama waamue
kuiunga kwani hakuna njia nyingine ya kutatua changamoto waliyonayo
zaidi ya kuwa wamoja.

No comments