Header Ads

Responsive Ads Here

CCM WILAYA YA GEITA YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI.


Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama cha mapinduzi Wilayani Geita wakiwa kwenye Mkutano wa kupitisha wagombea wa nyadhifa mbali mbali ndani ya chama.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Geita Barnabasi Mapande akiwasikiliza wajumbe ambao walikuwa wakizungumza kwenye Mkutano huo.

Mkuu wa Wilaya wa Wilaya ya Geita,alivaa kahunda Suti ,Pamoja na Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho ambaye yupo katikati.

Diwani wa Kata ya Kasamwa ,Merry Kasanda akichagia hoja iliyokuwa mezani kwenye Mkutano huo

Wajumbe wakifuatilia Kikao hicho.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola akisisitiza wananchi kuendelea kumuunga Mkono Rais wa Tanzania.

Mkuu wa Wilaya ya Geita akiwataka wananchama kuwa mstali wa mbele kujitoa kwenye swala la maendeleo katika kuchangia michango ambayo itawezesha shughuli za kimaendeleo.

Katibu  Mwenezi wa chama cha mapinduzi Wilayani Geita,Jonathan Masele akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za chama cha mapinduzi.
 

Chama cha mapinduzi CCM Wilayani Geita kimempongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Jitihada ambazo ameendelea kuzifanya ikiwa
ni pamoja na kufichua uovu kwa baadhi ya sekta za serikalini pamoja na
watumishi ambao wameendelea kuhujumu uchumi wa nchi bila ya kuwa na sifa za
kazi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake ,Katibu wa
siasa na uenezi  wa Chama hicho Wilaya humo Jonathani Masele ,amesema kuwa
shughuli na jitihada ambazo zimeendelea kufanywa na Rais Magufuli sio za
kubezwa na Watanzania kwani ni muda mrefu watu wamekuwa wakijifanyia mambo na
kujinufaisha Bila ya kuangalia manufaa ya Nchi.

“Tunatambua kazi ambazo anazifanya Mheshimiwa Rais sio za
kubezwa kabisa kama ambavyo tumeona miaka mingi Migodi ilikuwa ikisafirisha
mchanga bila hata ya watanzania kujua lakini yeye amefichua yote ambayo
yalikuwa yanaendelea Mimi namuomba Rais aangalie kwa wachimbaji wadogo kwani
baadhi yao wamekuwa na tabia ya kujibinafisisha maeneo mwisho wa siku
wanabadilisha majina bila hata ya kuyatumia maeneo hayo na ni vyema
wakanyangwanywa ili wapatiwe wale ambao wana uwezo wa kuendelea kuyatumia”Alisema
Masele.

Mwenyekiti wa  Wilaya Hiyo ,Barnabas Mapande akizungumza kwenye Kikao cha Halmshauri ya Wilaya ya chama hicho  amemtaka Rais kutokuwasikiliza
wale ambao wamekuwa wakimlalamikia na kwenda mbele zaidi ya Hapo ambapo
amefikia.

“Ni miaka mingi Watanzania wemeahangaika kwenye sekta nyingi
zikiwemo za afya na elimu lakini kwa sasa tunaamini kuwa mambo haya yote
yanakwenda kufanyiwa ufumbuzi kwa haraka zaidi mimi napenda kumshauri Rais
wangu aendelee na kazi ambayo anaifanya kwani ni nzuri kwa Watanzania wenye
hali ya chini”Alisema Mapande.

Mkuu wa Wilaya ya Geita  Mwl Herman Kapufi ambaye ni mmoja kati ya
wajumbe wa kikao hicho amewasisitiza wajumbe na wanachama kuwa mstari wa mbele
kwenye shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia kwenye maswala ya
elimu pamoja na afya huku akisisitiza kuwa yeye kama mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi
na Usalama Wilayani humo atahakikisha kuwa Mgodi ambao upo kwenye Wilaya ambayo
anaiongoza kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wanasimamia kwa
umakini dhahabu ambazo zinasafirishwa kwenda nje ya nchi.

Kamati ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM imekutana
leo lengo likiwa ni kujiandaa na uchaguzi ambao unatarajia kufanyika ndani ya
chama hicho.
 
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.

No comments