Header Ads

Responsive Ads Here

BULEMBO AUNGURUMA TABORA MJINI LEO, AZITAKA HALMASHAURI KUPELEKA FEDHA ZA MIKOPO KWA VIJANA NA KINAMAMA


 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdalla Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa Wilaya za Uyui na Tabora mjini, Viongozi wa CCM na watendaji wa Serikali, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Tabora, leo. Pamoja na kuzungumzia taratibu za uchaguzi ndani ya unaoendelea katika ngazi za mashina, Bulembo amewataka wana CCM, kutambua kuwa sare za CCM zina thamani kubwa kwa kuwa ni za Chama tawala hivyo wazivae hata wanapokuwa wanakwenda kutafuta huduma katika maeneo muhimu, Amewataka  pia madiwani kuhakikisha Halmashauri za wilaya zao zinatoa mgawo wa asilimia kumi fedha kutoka mapato yao, kwa ajili ya kuwapatika vijana na kina mama kwa ajili ya mikopo kwa kuwa utaratibu huo upo kisheria.

 ” Ndugu Bulembo Kazi hii ya Ukuu wa mkoa naipenda sana, hasa kwa sababu nasimamia ilani ya Chama changu, kwa niaba ya Wananchi wa mkoa huu, mpelekee Salaam, Mwenyetiki wetu, Rais Dk Magufuli, kwamba Tabora tunampongeza kwa kazi nzuri anazofanya, mwambie tuna imani naye na tutazidi kumuunga mkono”, akisema, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggry Mwanri alipotambulishwa kwenye kikao hicho
 Wajumbe wakionyesha bashasha na furaha kwenye kikao hicho
 Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggry Mwanri akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini, Mwalimu Queen Mwanshinga Mlozi, wakati wa mkutano huo
 Mkuu huyo wa Wilaya ya Tabora mjini akisalimia kabla ya kuangusha kigeregere cha aina yake ambacho kilisababisha wajumbe kushangilia kwa uhodari wake
 Kisha Mkuu huyo wa Wilaya ya Tabora mjini akahakinikiza kigeregere chake kwa kupiga magiti 
 Katibu wa Siasa na Oganaizesheni wa Jumuia ya Wazazi Makao Makuu, Ndugu Mgaya akisalimia wananchi baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho
 Msaidizi wa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Ndugu Kalolo akisalimia baada ya kutambulishwa
 Kishaa arindima kwa wimbo wa hamasa wa kabila la Wanyamwezi na baadaye kuporomosha mashairi yaliyosababishwa wajumbe kulipuka kumshangilia
 Wajumbe wakiwa wamesimama wakati Mchungaji Elias Mbagatwa alipokuwa akitoa dua maalum ya kumuombea Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli Mungu amjalie kuendelea kuchapa kazi na afya njema, wakati wa kikao hicho
 Mchuangaji Elias akiendelea na dua hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Kati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Ndugu Bulembo 
 Sheikh Hussein Mkamilwa wa Bakwata mkoani Tabora akiomba dua ya kubariki kikao kabla hakijaanza
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui Mussa Ntmizi akifungua kikao hicho
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Uyui Mussa Ntimizi akimkabidi Ndugu Bulembo zawadi ya asali
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora, Hassan Wakasubi akitoa maelezo ya matumizi sahihi ya asali kwa Ndugu Bulembo
 Kikao kikiwa kimefurika wajumbe, wakati Ndugu Bulembo akizungumza
 Wajumbe wa kikao hicho akifuatilia kwa makini
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdalla Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa Wilaya za Uyui na Tabora mjini, Viongozi wa CCM na watendaji wa Serikali, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Tabora, leo.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdalla Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa Wilaya za Uyui na Tabora mjini, Viongozi wa CCM na watendaji wa Serikali, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Tabora, leo.
 Madiwani wa Tabora mjini wakishangilia 
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdalla Bulembo akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa Wilaya za Uyui na Tabora mjini, Viongozi wa CCM na watendaji wa Serikali, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Tabora, leo.
 Ndugu Bulemo akisisitiza jambo
 Madiwani wa Uyui wakisimama kuulizwa maswali na ndugu Bulembo
 Mmoja wa wajumbe akifuatilia kwa makini kila kinachoendelea kwenye mkutano huo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdalla Bulembo akitoa ufafanuzi na kutoa maelekezo au maagizokuhusu maswali na kero zilizoulizwa na wajumbe kwenye kikao hicho, leo. Picha zote na Bashir Nkoromo

No comments