Header Ads

Responsive Ads Here

BREAKING NEWS; WANAFUNZI 33 NA WALIMU WAO WATATU WAFARIKI KATIKA AJALI ARUSHA; KAMANDA WA POLISI CHARLES MKUMBO ATHIBITISHA, LOWASSA ATUMA RAMBIRAMBI

Wasamaria wema wakijaribu kunasua miili ya wanafunzi iliyonasa kwenye mabaki ya basi  la shule lililotumbukia kwennye korongo la mto Malera, wilayani Karatu mkoani Arusha leo Mei 6, 2017.
 Wasamaria wema wakijaribu kunasua miili ya wanafunzi iliyonasa kwenye mabaki ya basi hikli la shule lililotumbukia kwennye korongo la mto Malera, wilayani Karatu mkoani Arusha leo Mei 6, 2017.
NA K-VIS BLOG, ARUSHA

BREAKING NEWS; Watu 30 wakiwemo wanafunzi 29, mwalimu mmoja na dereva wanahofiwa kufa baada ya basi la shule kutumbukia kwenye korongo  la mto Malera kwenye barabara ya Arusha kwenda Karatu kata ya Rhotia wilayani Karatu mapema leo asubuhi Mei 6, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, wanafunzi watatu wamejeruhiwa nakupelekwa kwenye hospitali ya Lutheran wilayani Karatu ikiwa ni pamoja na miili ya marehemu.

Wanafunzi hao wa darasa la saba kutoka shule ya msingi Lucky
Vincent ya Kwa-Mrombo jijini Arusha, walikuwa safarini kuelekea wilayani Karatu, kufanya mtihani wa ujirani wmema na wanafunzi wenzao wa shule ya msingi Tumaini.

Waheshimiwa wabunge kuna ajali mbaya sana imetokea mda huu eneo la kata ya Rhotia Wilaya ya  Karatu. Basi la wanafunzi wa St Lucky ya Arusha walikuwa wanaenda karatu kufanya mtihani na wanafunzi wenzao wa Tumaini English Medium School ya Karatu.
Habari zaidi zitawajia kadri tutakavyozipata. Miili ya wanafunzi wa shule ya msingi St.Vincent ya jijini Arusha ikiwa imelazwa baada ya kuondolwa kwenye basi hilo

No comments