Header Ads

Responsive Ads Here

BONANZA LA AFYA KWANZA LAFANA JIJINI ARUSHA


DSC09981
 wakwanza  kushoto ni muaandaji wa bonanza la Afya kwanza akiwa na timu ya Triple a klabu Fc  kabla ya mechi kuanza(habari picha na Woinde Shizza wa
libeneke la kaskazini )
timu ya tigo Fc ikiwa pamoja na timu
ya Triple A klabu FC 

 waimbaji wa bendi ya Ricker
nest music band wakiwa katika picha ya pamoja na rais wa bendi hiyo
alkievaa nyeupe
 wachezaji wa timu ya Triple a
wakiburudika mara baada ya mechi kuisha
 waimbaji wa timu ya Ricker nest
music band wakiwa na mmoja wa washabiki wao wa music wao wakifurahi
pamoja
 timu ya mringa ringa
iikiendelea kufanya mazoezi kabla ya kuingia
uwanjani
 timu ya wavuta kamba ikiendelea
kuvuta kamba
 warembo wakifuatilia mpira kwa
makini
 timu ya Triple A wakiwa
wanapeana mawazo katika kipindi cha mapunziko
 wadau mbalimbali waliouthuria
bonanza hilo wakiendelea kupata vinywaji
 mmoja ya wachezaji wa timu ya
Triple A klabu Fc akiwa anatolewa uwanjani na wauguzi mara baada
yakuumia wakati akicheza
 Timu ya Tigo Fc ikiwa katika picha ya
pamoja kabla ya mechi baina yao na timu ya Triple A Klabu Fc kuanza
Na Woinde Shizza,Arusha   

Timu ya Triple A klabu imelazimika kutoka sara ya bao moja kwa moja na timu ya Tigo FC  katika bonanza la michezo lijulikanalo kwa jina la Afya Kwanza
lililofanyika katika viwanja vya Gymkana jijini  hapa 
 

 Bonanza hilo ambalo ni mara ya kwanza kufanyika limeandaliwa na
mkurugenzi wa Bendi ya Rickernest music band ,bendi ambayo makao makuu
yake ni jijini hapa na imeshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta
kamba  pamoja na mpira wa miguu 
 
Akiongelea bonaza hilo muandaaji wa mashindano hayo Denis  Mtedeki   alisema kuwa nia rasmi ya kuandaa bonanza hili ni kuwakutanisha watu
mbalimbali  na kufurahi pamoja  pamoja na kushiriki michezo
,ikiwa kama ni sehemu ya kufanya
mazoezi 
 
Alisema kuwa bonanza hili limeshirikisha jumla ya timu za mipira wa miguu mbili pamoja na timu zingine mbili ambazo zilifanya kazi ya kuvuta kamba,alizitaja timu hizo kuwa ni
timu kutoka kampuni ya simu ya Tigo (Tigo Fc), Olemringaringa FC, Red Apple,Mijada Fc  pamoja na Triple a klabu FC.
 
 
Denis aliongeza kuwa mbali na kushiriki bonanza hili pia wachezaji na washiriki waliouthuria
walipata fursa ya kupima magonjwa mbalimbali ikiwemo kupima presha na kisukari
bure.
 
Aidha aliongeza kuwa bonanza hili alitaishia hapa bali
litakuwa likifanyika kila mwisho wa mwezi lengo ikiwa ni kufanya mazoezi
,kuwakutanisha wadau mbambali mbali na kufurahi pamoja
 

No comments