Header Ads

Responsive Ads Here

BENKI YA FBME YAFUTIWA LESENI NA BENKI KUU YA TANZANIA KUFANYA SHUGHULI ZA KIBENKI
NA K-VIS BLOG

BENKI Kuu ya Tanzania, (BoT), imeifutia leseni ya kufanya shughuli za kibenki, Benki ya FBME Bank Limited, kuanzia leo Mei 8, 2017 na kuiweka chini ya ufilisi.

Taarifa ya Benki kuu iliyotolewa Mei 5, 2017 na kusambazwa kwenye vyombo vya habari leo Mei 8, 2017 tayari imeteua Bodi ya Bima ya Amana kama mfilisi kuanzia leo hii Mei 8, 2017.

Aidha taarifa hiyo imewataka wenye amana, wadai na wadaiwa wawe wavumilivu wakati Mfilisi akiandaa utaratibu wa kushughulikia stahiki zao.

No comments