Header Ads

Responsive Ads Here

Atengeza kitabu cha Quran cha mita 700 kwa mkono Misri


Saad Mohammed ametumia miaka mitatu akitengeza Quran hiyoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionSaad Mohammed ametumia miaka mitatu akitengeza Quran hiyo
Raia mmoja wa Misri aliyewacha shule anatumai kuweka historia baada ya kutumia muda wa miaka mitatu akitengeza kile kinachoonekana huenda ikawa Quran kubwa zaidi duniani.

Quran hiyo inayotengezwa na Saad Mohammed ambayo ameipamba, ina urefu wa mita 700 ikimaanisha kwamba inapofunguliwa ina urefu wa mita 381 sawa na jumba la Empire State.
Na kufikia sasa bwana Mohammed anayeishi katika mji wa Belqina kaskazini mwa Cairo amefadhili kila sentimita ya mradi wake.
Lakini ana matumaini makubwa .
Mtu huyo aliyewacha shule pia ameandika vitabu nyengineHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMtu huyo aliyewacha shule pia ameandika vitabu nyengine
Itakuchukua takriban dakika tano kutembea urefu wa kitabu hichoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionItakuchukua takriban dakika tano kutembea urefu wa kitabu hicho
Anaamini kwamba kitabu hicho ni kirefu mno kuvunja rekodi za Guiness World Records ambapo hakuna rekodi iliowekwa ya Quran ndefu zaidi ilioandikwa kwa mkono.
Lakini ili kiafikia ndoto yake na kufanikiwa katika vitabu hiyo vya rekodi za Guiness anataka usaidizi wa gharama ya kuingia katika shindano hilo.
''Quran hii ina urefu wa mita 700 na kwa kweli hiyo ni karatasi kubwa sana'', aliambia runinga ya Reuters.
''Nimejidhamini mwenyewe na mimi ni mtu wa mapato ya kawaida.Sina mali ama chochote kile''.
Mr Mohammed amfadhili gharama yote ya kutengeza Quran hiyoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMr Mohammed amfadhili gharama yote ya kutengeza Quran hiyo
Gharama ya kununua karatasi alioandikia ni kubwaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionGharama ya kununua karatasi alioandikia ni kubwa
Lakini ana matumaini ya kupata ufadhili ili kuingia katika shindano la rekodi za Guiness dunianiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionLakini ana matumaini ya kupata ufadhili ili kuingia katika shindano la rekodi za Guiness duniani

No comments