Header Ads

Responsive Ads Here

ALEX MSAMA AKERWA NA HABARI ZA KUMCHAFUA YEYE NA FAMILIA YAKE


1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mtaa wa Mkwepu Posta jijini Dar es salaam wakati akielezea habari ya gazeti moja la wiki lililoandika kwamba amefilisika na anatafutwa na mahakama huku akiwa amekimbilia kusiko julikana.

Msana amesema yeye ana kampuni nyingi tu anakwenda ofisini kwake kila siku na anawafanyakazi ofisini hajaoni mtu yeyote kutoka Mahakamani akileta ujumbe wa yeye kuitwa mahakamani, lakini pia hakuna hata taarifa ya yeye kuitwa polisi kwa tuhuma yoyote hivyo habari hizo ni za uzushi na zinalenga kumpaka matope, lakini baya zaidi zinahusisha familia yake.
Amesema anajadiliana na wanasheria wake ili kuwafikisha mahakamani wahusika kwa sababu wamelenga kumvunjia heshima yeye, kampuni zake na familia yake mbele ya jamii ya watanzania.
Amemaliza kwa kazi ya kuandaa utaratibu  utakapokamilika watapeleka mashtaka mahakamani ili kudai haki yake ya msingi udhalilishaji uliofanywa na wahusika hao.
2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana
3
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akionyesha kukerwa na habari hizo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam jana

No comments