Header Ads

Responsive Ads Here

Utafiti: Kerengende wa kike ''hujiuwa'' ili kukwepa tendo la ngono


Kerengende wa kike hujifanya wamekufa ili kukwepa tendo la ngono na wenzao wa kiumeHaki miliki ya pichaJOHN MURRAY
Image captionKerengende wa kike hujifanya wamekufa ili kukwepa tendo la ngono na wenzao wa kiume
Utafiti mpya umebaini kwamba kerengende wa kike huwa anajifanya kuwa amekufa ili kukwepa wenzao wa kiume.

Rassim Khelifa, kutoka chuo kikuu cha Zurich Switzerland, anasema kwamba aliona kerengende wa kike aliyekuwa akifuatwa na wa kiume ili kufanya mapenzi, akijiangusha na kulala kana kwamba amefariki, hadi pale kerengende wa kiume alipoondoka.
Ripoti hiyo imechapishwa kwenye jarida la ikolojia.
Bwana Khelifa amsema kuwa kerengende wa kike hunyanyaswa kwa sababu huwa hawana ulinzi baada ya kutaga mayai ikilinganishwa na kerengende wengine.

No comments