Header Ads

Responsive Ads Here

Mume na mke waliooana miaka 69 wafariki pamoja Marekani


Wawili hao walikuwa wameoana kwa miaka 69Haki miliki ya pichaHISANI
Image captionWawili hao walikuwa wameoana kwa miaka 69
Wanandoa wawili katika jimbo la Illinois, waliokuwa wameoana kwa miaka 69, walifariki wakiwa wameachana kwa saa moja pekee, jamaa zao waliambia vyombo vya habari Marekani.

Isaac Vatkin, 91, alikuwa amemshika mkono mkewe Teresa, 89, alipofariki kutokana na ugonjwa wa Alzheimer Jumamosi, gazeti la Daily Herald.
Isaac alifariki dakika 40 baadaye.
Jamaa zao walisema walifarijiwa kwamba wawili hao walikuwa pamoja hadi mwisho.
"Hungelipenda kuwaona wakituacha," alisema mjukuu William Vatkin, "lakini hungetaka zaidi ya hilo."

No comments