Header Ads

Responsive Ads Here

MAOMBI YA USAJILI WA WAKALA BINAFSI WA HUDUMA ZA AJIRA KWA KIPINDI CHA 2017/18


      index

 1. Kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 20 cha Sheria ya Kukuza Huduma za  Ajira 9 ya Mwaka 1999 pamoja na Kanuni zake kupitia Gazeti la Serikali Na.232 la tarehe 11Julai 2014, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu inakaribisha maombi  kutoka Makampuni yanayotaka kufanya shughuli za uwakala binafsi wa huduma za ajira kwa kipindi cha mwaka 2017/18
 1. Miongoni mwa majukumu ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira ni pamoja na kuunganisha Watafuta kazi na Waajiri pasipo kuwa sehemu ya mahusiano ya kiajira yanayoweza kujitokeza baina ya Watafuta kazi na Waajiri; na  kutoa huduma zingine zinazohusiana na utafutaji kazi kama vile kutoa ushauri wa ajira na taarifa za soko la ajira kwa Watafuta kazi na waajiri. Aidha, waombaji wa Uwakala ni vema wakaainisha sekta wanazopenda kufanyia kazi kama Wakala  Binafsi wa Huduma za Ajira.
 1. Ifahamike kuwa kwa kusajiliwa kuwa Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira  hataruhusiwa kufanya ukodishaji wa watu (outsourcing of persons) yaani Kuajiri na Kukodisha Wafanyakazi,  kuajiri kwa niaba ya kampuni nyingine, na kuwa sehemu ya Mahusiano ya ajira ya Watafuta kazi na Waajiri
 1. Kampuni zinazoomba Usajili zinatakiwa ziwasilishe maombi pamoja na nyaraka zifuatazo:
 2. Barua ya maombi;
 3. Katiba ya uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kampuni (Memorandum&Articles of Assocition).
 • Hati ya usajili wa kampuni (Certificate of incorporation).
 1. Hati ya usajili wa Jina la Biashara (Business name)
 2. Leseni ya Biashara(Business License).
 3. Namba ya usajili wa mlipa kodi (Tax identification Number).
 • Wasifu wa Kampuni au Wakala pamoja na ujuzi na uzoefu wa wataalamu katika uendeshaji wa huduma za ajira (Company profile).
 • Uthibitisho wa Kampuni au Wakala katika kulipa kodi (The current tax clearance letter from Domestic revenue/larger tax payers department)
 1. Anuani kamili ya makazi (Permanent physical address) pamoja mkataba wa pango la ofisi

 1. Maombi yote ya usajili yawasilishwe  ofisi ya  Kamishna wa Kazi iliyopo  jengo la Mwalimu Nyerere  Pension Tower, Barabara ya Bibi Titi Mohamed,  S.L.P. 1422,  Dar es salaam.
 2. Maombi yawasilishwe ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu kutolewa kwa tangazo hili na tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi itakuwa ni tarehe 30/5/2017. Maombi   yaambatane na ada  ya usajili ya kipindi cha mwaka mmoja isiyorudishwa  ya kiasi cha  TSHS. 500,000 (Laki tano tu).

Imetolewa na:

Kamishna wa Kazi
Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana, Ajira, na  Wenye Walemavu.

27.04.2017

No comments