Header Ads

Responsive Ads Here

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA KUZINDUA MRADI WA MAJI KATIKA WILAYA YA UYUI MKOANI TABORA

mak2
Na Tiganya Vincent-RS-Tabora.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama katika kijiji cha Mabama wilayani Uyui mkoani Tabora.

Taarifa hiyo imetolewa leo mjini Tabora na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mkuu wa Wialaya ya Tabora Queen Mlozi imesema kuwa sherehe za uzinduzi wa mradi huo zitaanza asubuhi siku ya Jumamosi ya tarehe 29 Mwezi huo.

Amesema kuwa baada ya uzinduzi wa mradi huoi , Makamu wa Rais atapata fursa ya kuwahutubia wananchi na viongozi mbalimbali katika viwanja vya Shule ya Msingi Mabama.

Aidha , Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora ametoa wito kwa viongozi wa dini zote, vyama vyote vya siasa, viongozi wa serikali na wananchi wa maeneo yaliyopo karibu na mradi huo kujitokeza kwa wingi kwenda kusikiliza hotuba ya Makamu wa Rais.

Uzinduzi wa mradi huu utasaidia kuondoa tatizo la maji safi na salama kwa wakazi wa eneo hilo na ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwaondole matatizo mbambali wananchi likiwemo la upatikanaji wa maji safi na salama.

Mradi  huo wa maji ambao umefadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan(JICA) umewezesha umesaidia uchimbaji wa visimana ujenzi mitandao ya mabomba katika eneo hilo wilayani Uyui.

No comments