Header Ads

Responsive Ads Here

BOCCO ATAMBA MAPEMA TU SIMBA ITAPIGWA TAIFA JUMAMOSI


18118691_1607195839320766_1552364098670607677_n
 
Nahodha wa Azam FC, John Bocco ameendelea na mazoezi na wenzake na sasa anaonekana yuko tayari kwa mechi ya Jumamosi dhidi ya Simba.

Simba na Azam FC zitakutana Jumamosi katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Tokea Bocco ameungana na wenzake baada ya kufanya mazoezi chini ya uangalizi wa daktari amekuwa akionekana kuimarika zaidi na sasa anashiriki mazoezi akionyesha keshokutwa, atakuwa mzigoni.
Nahodha huyo wa Azam FC, amekuwa gumzo kati ya wachezaji ambao mashabiki wengi wangependa kumuona akiwa uwanjani katika mechi hiyo.
Hivi karibuni, Bocco alipata bahati mbaya ya kuandamwa na majeraha mara kwa mara, hali iliyosababisha kukosa mechi kadhaa.

No comments