Header Ads

Responsive Ads Here

WANAWAKE WAUNGANA KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KATIKA VIWANJA VYA MWEMBE YANGA DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi wa IBRA Contractors na Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET), Maida Waziri akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam kabla ya Mgeni rasmi kuzungumza.
 Wanakikundi cha Vicoba Endelevu wakiwa wamesimama na bango lao katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani


 Mkurugenzi wa IBRA Contractors na Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET), Maida Waziri aliyebebwa na baadhi ya wanawake waliojawa na furaha baada ya kuelezea historia yake ya mafanikio iliyowasisimua wengi katika uwanja wa Mwembe Yanga Jijini Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani
 Mkurugenzi wa IBRA Contractors na Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET), Maida Waziri aliyebebwa na baadhi ya wanawake waliojawa na furaha baada ya kuelezea historia yake ya mafanikio iliyowasisimua wengi katika uwanja wa Mwembe Yanga Jijini Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani

 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza katika Maadhimisho Dar es Salaam leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
 Mwanahabari wa Mtembezi Blog akiwajibika
 Akina mama katika muonekano pichani wakifatilia kwa umakini wakiwa na bango lenye ujumbe maalumu
 Mwanahabari akidadisi jambo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Farijika Production, Nipael Kamwava inayo jishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa dawa mbalimbali za asili za Binadamu
 Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), wakiwa katika picha ya pamoja katika Maadhimisho ya Wanawake Duniania
 Baadhi ya wafanyakazi wanawake Wizara ya Ulinzi na Jeshi  la Kujenga Taifa wakipita mbele ya jukwaa kuu wakati wa kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Machi 8, 2018.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake Wizara ya Ulinzi na Jeshi  la Kujenga Taifa, Salma Omary akizungumza na wanahabari wakati wa Maadhimisho hayo alisema, katika kuondoa changamoyo zinazo jitokeza katika kutatua maswala mbalimbali, inahitaji sana ushirikiano wa wanawake wenyewe kwa wenyewe na kujitabua kwamba wao ni akinanani ili waweze kuondoa hizo changamoto kwa kukaa pamoja na kujadili kwa pamoja na ndipo kunaweza kupatikana mafanikio, pia akitowa wito kwa akinamama wote kwa kujiamini, wasikate tamaa na mahali amapo pana utata anachangamoyo nyingi za kutosha asisite kuwaona wanawake wenzake kama, jumuiya za wanawake sehemu mbalimbali kama vijijini na mijinina akasema kama sehemu za ibada na anaweza kupeleka changamoto hizo zinaweza kupatiwa ufumuzi na hata kwa mawazo kuliko kujifungia ndani na hatimaye kukata tamaa 
Mkurugenzi wa Cliniki ya Tiba wa Kituo cha Jikwamue Asili Production, Hamisi Haruna (kushoto) akitowa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  yaliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo wakati alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

No comments