Header Ads

Responsive Ads Here

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA MIKOA YA SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA

 Mtoto akiswaga ng'ombe Sheluhi mkoani Singida wiki iliyopita kama alivyonaswa na kamera yetu. Watoto kama huyu wakijengewa mazingira mazuri ya kupata elimu wanaweza kuwa wataalamu wa ufugaji wa kisasa.
 Kondakta wa Fuso lenye namba T 389 AZN, akiangalia gari lake lililopata ajali Kijiji cha Nanga wilayani Nzega mkoani Tabora, wiki iliyopita. Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyepoteza maisha.
Wanawake wa Kahama mkoani Shinyanga wakiuza maembe kando ya barabara wiki iliyopita jambo linaloweza kuhatarisha usalama wao iwapo gari litaacha njia.
 Waendesha pikipiki 'bodaboda' wakikiuka sheria ya usalama barabarani kwa kupakia abiria kwa mtindo wa watu watatu jirani na Pub ya Masai wilayani Kahama mkoani Shinyanga jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.
Wanyama kazi wamekuwa wakisaidia katika shughuli za kilimo kwa kubeba mizigo kama punda huyo anavyoonekana akikokota mkokoteni unaotumika kubebea mizigo na mazao maeneo ya Tinde wilayani Nzega mkoani Tabora, wiki iliyopita. (Picha na www.mwaibale.blogspot.com)

No comments