Header Ads

Responsive Ads Here

MWANAFUNZI WA CHUO CHA UALIMU ST. AGREY MBEYA AUAWA BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA PIKIPIKI

kumradhi kwa kuzitumia picha hizi
Hii ndiyo pikipiki inayodaiwa kuibwa na mwanafunzi huyo.


Hiki ni kitambulisho cha mwanafunzi huyoMwanafunzi wa Chuo cha Ualimu cha ST Aggrey, kilichopo Uyole nje kidogo ya jiji la Mbeya anasadikiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali katika maeneo ya Isanga akidaiwa kuiba pikipiki zakusafirishia abiria maarufu kama bodaboda.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Pray God Mgonja amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Vedasto Pius anayekadiriwa kuwa na umri kati 25 mpaka 30 .

Mgonja amesema tukio hilo limetokea Julai 2 mwaka huu saa 8 za mchana katika daraja lilopo karibu na Hotel ya Rift Valley barabara yakuelekea Isanga jijini mbeya.

Amesema mtuhumiwa amekumbwa na mkasa huo baada yakupewa taarifa za kuibiwa kwa pikipiki yenye No T 438BZU aina T-BETTER yenye alama ya chama cha Demokrasia na maendeleo mali ya Joseph Kapasi(23), mkazi wa Ilomba.

 
Kwaupande wake mmiliki wa pikipiki hiyo Joseph Kapasi amesema aliombwa kumfundisha mtuhumiwa huyo na baadae alipoanza kuendesha vizuri alitokomea nayo na mara baada ya hapo alipatikana eneo la Isanga akielekea barabara ya chunya ili aibe na ndipo akakamatwa na wananchi wenye hasira kali nakuanza kumpa kichapo ambacho kilimfanya apoteze fahamu na baadaye kudaiwa kufariki dunia.
Hata hivyo jitihada za kumpata Mkuu wa Chuo hicho ili kuthibitisha kama ni kweli mwanafunzi alikuwa akisoma katika Chuo hicho zilishindika hata hivyo jitihada hizo zinafanyika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi (ACP), Athuman Diwani hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo

No comments