Header Ads

Responsive Ads Here

PPRA YACHARUKA YAZIFUNGIA KAMPUNI 34

Ofisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dk. Ramadhan Mlinga, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam , wakati akitoa taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi wa PPRA kuzifungia Kampuni 34 kutoshiriki katika zabuni za Taasisi za Umma kwa kipindi cha mwaka mmoja. Kulia ni Mwenyekiti wa hiyo, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo. (PICHA NA DOTTO MWAIBALE)


PPRAA yacharuka yazifungia kampuni 34

Na Dotto Mwaibale

MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), imecharuka kwa kuyafungia makampuni 34 kutoshiriki katika zabuni za Taasisi za Umma kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia jana.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dk. Ramadhan Mlinga, alisema hatua hiyo ilifikwa katika kikao kilichoketi jana.

"Hatua hii imefikiwa katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi cha PPRA kilichoketi jana chini ya Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Thomas Mihayo" alisema Dk. Mlinga.

Alisema kufungiwa kwa kampuni hizo ni kwa mujibu wa kanuni namba 102 (2) ya Tangazo la Serikali namba 97 la mwaka 2005.

Aliongeza kuwa kati ya Kampuni hizo, 26 zimefungiwa baada ya kushindwa kutekeleza mikataba yao na Taasisi husika na hivyo kusimamishwa kutekeleza mikataba hiyo.

Alizitaja kampuni zilizofungiwa kuwa ni Lemungo Contruction Co. Limited, Majajulu Investment Limited, Ostrich Maintenance Works Limited na Nzori General Enterprises Limited.

Nyingine ni Commetech Contractors Limited, Niako Supplies Company Limited, Shedol Construction Limited, Maktech &Tel Company Limited na Jimmy Money Enterprises.

Dk. Mlingwa aliyataja Kampuni zingine kuwa ni Zephania Ngeleja of Ukerewe, Mawson Construction Limited, Mahende Garage and Construction Co.Limited, Nyanda & Company na Kipusi Traders.

Kampuni zingine ni Jawabu Construction Company Limited, Mike Construction, Rana Decoration, Buildingand Civil Contractor, Grace Mbilinyi na Computech ICT (T) limited.

Alizitaja Kampuni zingine kuwa ni Girland Developers Limited, Camsa Construction Company Limited, Twabaha Construction Company Limited na Malaika Building Construction and Civil Work.

Kapuni zingine ni Mussa Mbweso, Ligero Construction Company Limited, Julius Mwamlima Construction, Muson Engineer Limited na Man-Ncheye Pa Company Limited.

Nyingine ni F.I.C Limited, Nyegezi JJ Construction Limited, Jassam and Company Limited, Satelite Construction Ltd, Icon Engineer na Tengo Construction Ltd.

Katika hatua nyingine Dk. Mlinga alisema Bodi hiyo ilijadili kuhusu watendaji ambao Taasisi zao hazikufanya  vizuri katika ukaguzi wa mwaka 2010/11 na zile zilizoshindwa kuandaa mafunzo kwa wakufunzi kutoka PPRA kwa ajili ya kujifunza na kujadili maeneo ambayo wanamatatizo nayo.

Alizitaja Taasisi hizo kuwa ni Tanzania Coffee Board, Baraza la Kiswahili la Taifa, Urambo District Council, Mtwara Urban and Sewarage Authority na High Court of Tanzania.

Taasisi nyingine ni Air Tanzania Corporation, Mkinga District Council, Igunga District Council, Singida Manicipal Council, Sengerema District Council na Ilala Municipal.

Dk. Mlingwa alizitaja Taasisi zingine kuwa ni Prisons Department, Ministry of Home Affairs, Masasi District Council, Uwasa Morogoro na Tanzania Ports Authority na Institute of Judicial Administration.

Zingine ni Contractors Registration Board, Kilolo District Council, Kilombero District Council, Nachingwea District Council, na Tanzania Cotton Board.

Alitaja Taasisi zingine kuwa ni Lindi Urban Water and Sewarage Authority, Kinondoni Municipal Council, Magu District Council, Mvomero District Council, Tunduru District Council, Temeke Municipal Council, Same District Council na Tanesco.

Dk. Mlingwa alichukua fursa hiyo kuzitadharisha Kampuni mbalimbali kuwa hazita kuwa tayari kushirikiana na PPRA katika kufanikisha lengo hilo Umma usitegemee matokeo hayo ya ufujaji wa fedha katika taarifa ijayo ya ukaguzi ya PPRA.

No comments