Social Icons

b

b

w

w

.

Sample Text

Pages

Featured Posts

Thursday, October 27, 2016

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS OKTOBA 27


WASICHANA WASOMI 14 WAZALENDO WAONYESHA UWEZO NCHINI TANZANIA WASEMA MWANZO WA TANZANIA MPYA UMEANZA


Picha ya pamoja ya wasichana 14 waliojitolea kufanya kazi ya kufyatua matofali kusaidia ujenzi wa mabeni na nyumba za walimu katika shule ya sekondari Nasibugani.

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Felbeto Sanga wa kulia,akizungumza na baadhi ya wadada walijitolea kufanya kazi hiyo.


baadhi ya matofali yaliyo fyatuliwa na vijana hao waliojitolea

Moja ya chumba kinachotumiwa na wanafunzi hao kulala kwa kuweke magodoro chini.
 Moja ya Bweni linalotumiwa na wanafunzi shuleni hapo linavavyoonekana.Mwezi mmoja uliopita vijana wazalendo walitembelea Shule ya Sekondari ya Nasibugani umbali wa KM 98 toka Dar es salaam,iliyoko Mkoa wa Pwani wilaya ya Mkuranga kwa wito wa Mkuu wa wilaya hiyo Filbeto Sanga,ikiwa na umbali wa KM 53 vijijini ndani kutoka makao makuu ya wilaya hiyo kujionea kile kinacho wasibu Wadogo zao wasomi walioko shuleni hapo.

Walikuta chumba kimoja chenye vitanda viwili vya upana wa futi 2,2 wanalala Wanafunzi wawili wawili,chumba kimoja cha wastani chumba kilichokuwa Maabara wanalala watoto tena magodoro yakiwa chini wanafunzi 70,walikuta nyumba moja ya Waalimu yenye vyumba vitatu wanaishi waalimu 7
Tangu wiki hiyo ya tarehe 27/9/2016 hadi unasoma ujumbe huu,Wadada hawa Wazalendo na wasomi hawakurudi nyumbani,wanaikataa hali hiyo kwa vitendo kama suluhisho pekee la matatizo makubwa ya makaazi na mabweni ya Shule nyingi hapa nchini,wanashiriki kwa kujitolea ujenzi wa mabweni matano na nyumba tano za waalimu zitakazo kidhi upungufu katika Shule hiyo.Hamasa hii imewapa changamoto kubwa vijana wa kiume 39 walioamua kuungana na Wakinadada  14 hadi unasoma uzi huu Tayari wamekwisha fyatua Matofali 45,000 yanayokidhi Mabweni matano na nyumba tano za Waaalimu 
Vijana hao wanakula chakula kile kile wanachokula wanafunzi hawo,na kuisha mazingira kama  wanafunzi,
Serikali Mkoani Pwani inasema haijawahi kutokea kwa Miongo mingi ya Umri wa Taifa hili:
Akizungumza mmoja wa kijana aliyejitolea Happines Komba amesema kuwa ameamua kujitolea kufanya kazi ili kusaidia shule hiyo kupata majengo yatakayo wawezesha wanafunzi kuishi katika mazingira mazuri.
“nimepata nafasi ya kusoma na kumaliza chuo nikaona nina kila sababu ya kutumia nguvu zangu kusaidia kazi za jamii nimesukumwa na uzalendo kuja huku kufanya hiki kwa ajili ya taifa”alisema Bi Komba
Ameongeza kuwa vijana wanapaswa kuwa wazalendo kwa kulitumikia taifa na kuacha kuchangua kazi kwani kwa kufanya hivyo ni kurudisha nyuma maendeleo ya taifa,na kuongeza kuwa vijana kuamka na kufanya kazi.
“mimi ni dada nina shahada kutoka chuo cha IFM nipo huku tunafyatua matofali na kwa siku tunafyatua matofali mpaka 2000 kwa siku kwahiyo wadada wasijiweke nyuma”alisema Komba Kwa upande wake Rosemunda Mgimba aliyemaliza chuo kikuu cha dare s salaam na kupata shahada ya sayansi ya siasa,alisema kuwa amejitoloea baada kusikia taarifa ya shule hiyo wanafunzi kulala kwa shida kutokana na kukosa mabeni ya kutosha.
“niliumia sana kusikia wadogo zetu wanapata shida ya kulala na wako shule nikaona nina uwezo wa kufanya kitu kwa ajili ya nchi yangu na ndio sababu nipo huku kusaidia kutatua tatizo sikutaka kuwa sehemu ya kulalamika bali kutenda.’alisema RosemundaAidha aliongeza kuwa vijana wawe na moyo wa kujitolewa kwa kuangalia matatizo ya nchi na kuwakumbusha kuwa wanawajibu wa kulitumikia taifa kwa ajili ya faida ya wengine na kutumia muda wao kutatua changamoto zilizopo zinazohitaji nguvu kazi.
Naye Petro Magoti amesema kuwa wameguswa na kuamua kuweka kambi katika shule hiyo ili kusaidia kumaliza tatizo hilo kwa kutumia nguvu kazi inayoshirikisha vijana 53 huku 14 wakiwa ni wanawake.“kwa kweli mambo yamebadilika sana ukiangalia hapa kuna wadada 14 ambao tumekaa nao huku kufanya kazi hii ya kufyatua matofali na wanafanya kazi kubwa sana kusaidia taifa letu”alisema Magoti Magoti amesema kuwa shule hiyo imezidiwa na wingi wa wanafunzi na kuamua kutumia nguvu kazi katika kusaidia serikali kutatua changamoto hiyo,na kuongeza kuwa wamefyatua matofali zaidi ya elfu 45,000 kwa ajili ya ujenzi huo.
“imefika wakati vijana kujiuliza wanataka kufanyia nini taifa lao na sio taifa limewafanyia nini” alisema Magoti Kwa upande wake Lulu Kamaramo aliyesoma chuo kikuu nchini Malysia aliesema kuwa uzalendo ndio kitu muhimu katika nchi kwani ndio uliomfanya kufanya kazi hiyo bila kujali elimu aliyokuwa nayo.“vijana tujifunze uzalendo ili kusaidia seriikali kwani Rais wetu anajitahidi kufanya kazi ya kutuletea maendeleo tuna kila sababu ya kufanya kazi hizi kwa kutumia muda wetu na nguvu tulizonazo”alisema Lulu

Mtendaji wa Kata aswekwa Rumande kwa Matumizi mabaya ya Fedha za Umma

   Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi, Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya Ngorongoro wakionyesha  zana  walizotumia kutengeneza barabara  ya Km 24 kwa nguvu zao wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Mrisho Gambo  katika  Kijiji hicho.
  Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi, Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya Ngorongoro wakishangilia Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ulipokuwa unawasili katika Kijiji hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(Mbele kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo(Mbele  Kulia) wakiwasili  kwenye Mkutano wa hadhara  katika Kijiji cha  Esokonoi.
 Mwenyekiti  wa CCM Mkoa wa Arusha  Mhe. Michael Lekule Laizer akiongea na wananchi wa Kijiji cha  Esokonoi wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa katika Wilaya hiyo.
 Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi wakimskilizia Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Mrisho Gambo (hayupo pichani) alipokua akizungumza nao kwenye Mkutano wa hadhara.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mhe. Michael Lekule Laizer(kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  (Katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido wakiwa katika mavazi ya asili ya Kimasaai waliyovishwa kwa heshima na wananchi wa Esokonoi.


Nteghenjwa Hosseah – Longido

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Londifo, Juma Mhina ameamuru polisi wa Wilaya hiyo kumkamata na kumuweka ndani Mtendaji wa Kata ya Gilai Lumbwa, Paul Lucas baada ya kutuhumiwa kutumia Fedha za umma vibaya zilizochangwa na wananchi wa maeneo hayo kwa ajili ya kuinua Sekta ya Elimu.

Agizo hilo la Mhina lilifanikiwa baada ya mara kwa mara kushindwa kumkamata Paulo baada ya kumkwepa kila alipokuwa akitafutwa na hatimaye mtendaji huyo kujitokeza kwenye Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisgo Gambo uliofanyika kwenye Kijiji cha IIchang Sapukin kata ya Gilailumbwa.

Mmoja kati ya wananchi walioshirki Mkutano huo Bi. Anni Mollel alimshukuru Rc Gambo kufika Kijijini hapo na kujionea hali halisi ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ambayo wananchi walichanga Fedha zao zaidi ya Tsh Mil 96 ila hazikutumika kama ilivyokusudiwa badala yake viongozi wa Serikali na Wenyeviti wa Kijiji walitumia Fedha hizo kujinufaisha binafsi badala ya kuwasaidia watoto kukaa kwenye mazingira mazuri ili wapate Elimu.

“Yaan bora umekuja Mkuu hawa viongozi wetu huku kijijini ni Miungu watu wanajipangia mambo yao ya kubadilisha matumizi ya Fedha zilizochangwa na wananchi kaka zao yaan ukiwaangalia wao wana maisha mazuri wakati sisi tunateseka sasa lro uondoke nao na tunamuomba Mkurugenzi wa Halmashauri hii Ndg. Mhina kuwaleta watumishi wengine na wale waliohamishwa hapa baada ya kushirki kula hela zetu wakamatwe pia na waseme wamepeleka wapi hela zetu”

Mara baada ya wananchi kusema hayo Gambo alimhoji Mkurugenzi Mhina ni kwa nini hawajachukua hatua za kisheria kuwakamata watuhumiwa ndipo Mhina aliposema mbele ya hadhara hiyo kwamba zoezi hilo lilishindikana awali baada ya Paulo kumkwepa Mkurugenzi huyo mara kwa mara lakini jana alijileta mwenyewe katika mkutano huo na ndipo imekuwa rahisi kwake kumkamata.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkaguzi wa ndani wa Halmahauri hiyo, Bi. Mwajuma Mndaira kwenye Mkutano huo alidai kuwa alifanya mahojiano na wenyeviti wa vijiji kujua ni kwa nini walikusanya Fedha kwa wananchi bila kutumia stakabadhi za Serikali katika zoezi hilo.

Pia hivi sasa bado wananendelea na uchunguzi wa nyaraka za malalamiko mbalimbali ili kubaini Paulo alihusika na kinanani na kwa nini abadilishe baadhi ya matumizi ya Fedha hizo na kuuza baadhi ya vitu vilivyochangwa bila kuonyesha sababu ya Msingi kwani baadhi ya kampuni za uwindaji wa kitalii ikiwemo Wingert WindroseSafaris na Kampuni ya Kilombero Nothern Safaris zilitoa mifuko ya Saruji 400 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari hiyo.

Rc Gambo alimuhoji Mtendaji huyo kwanini shule hiyo haijakamilika mpaka leo wakati watoto wa jamii ya kifugaji wana haki ya Kupata Elimu na wazazi wao wanajitoa wa ajili ya watoto wao huku yeye akiendelea kuwarudisha nyuma, Paulo alijitetea kwamba baadhi ya fedha hizo ziliztumika kihalali na fedha zingine alilazimik kubadilisha matumizi yake na kujenga vyumba vya maabara, jiko pamoja na mabweni,

Baada ya utetezi wake kugonga mwamba alijikuta yupo chini ya himaya ya Polisi waliokuwa wakiongoza msafara huo ambapo pia Mkuu wa Wilaya hiyo Chongolo aliahidi wananchi hao kuwa atafuatilia suala la watumishi wengine watakoziba nafasi za wote watakaomatwa na ubadhirifu huu kuletwa haraka iwezekanavyo ili huduma zisizorote na endapo tuhuma hizi zikithibitkka watapelekwa Mahakamani na aliongezwa kuwa atakua karibu nao kuhakikisha kero kama hizo hazijitokezi rena hapo baadae . 

DKT. MGWATU AWATAKA WATENDAJI KUZIBA MIANYA YA UPOTEVU WA MAPATO TEMESA


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu  wa kwanza kushoto akiangalia “honing machine” inayotumika kituoni hapo, kulia kwake ni ndugu Firmin Lyaruu na Meneja wa TEMESA Kilimanjaro Mhandisi Alfred Ng’hwani.


NA THERESIA MWAMI- TEMESA KILIMANJARO.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka watendaji kuziba mianya ya uvujaji wa mapato, ili kuhakikisha Wakala unakusanya mapato iliyokusudia na kufanya matumizi stahiki kwa maendeleo ya Wakala.

Amesema hayo wakati akizungumza na  na watumishi wa kituo cha TEMESA Kilimanajaro alipotembelea na kujionea hali ilivyo katika kituo hicho na kuwahimiza watumishi wa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja na kutoa huduma zenye ubora. 

“Nawaomba muwe na  mbinu mbadala yakuzuia mianya ya uputevu wa mapato na  mzibane Taasisi mnazozidai  walipe madeni ili mapato yatakayokusanywa yasaidie kuboresha zaidi karakana zetu.” Alisisitiza Dkt. Mgwatu. 

Nao watumishi wa kituo cha TEMESA Kilimanjaro kwa nyakati tofauti, wamemuahakikishia mtendaji huyo kufanya kazi kwa kujituma na kuzidi kupambana kuipeleka mbele TEMESA ingawa kumekuwapo na  ukosefu wa vitendea kazi  kulingana na taaluma mbali mbali zilizopo kwenye kituo hicho.

Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vilivyopo kanda ya Kaskazini kuangalia utendaji kazi wake na kuona changamoto zilizopo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa maendeleo ya Wakala huo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akipata maelezo ya utendaji kutoka kwa Meneja wa TEMESA Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Ng’hwani alipotembelea kituoni hapo.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wakwanza kulia), akiongea na watumishi wa TEMESA Kilimanjaro alipotembelea kituoni hapo

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WANNE KUTOKA NCHI MBALIMBALI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa India nchini, Sandeep Arya (kulia) mara baada ya Balozi huyo kumaliza mazungumzo na Waziri ambayo yalifanyika ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Mazungumzo hayo yalikuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India. (Picha na zote Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Balozi wa India hapa nchini, Sandeep Arya (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Norway
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Rwanda, Eugene Kayihura (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kushoto) kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Norway na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. 

MADJZ WA LAKE FM KUDONDOSHA BURUDANI TAMU KWENYE USIKU WA MSHIKE MSHIKE JIJINI MWANZA LEO.


Burudani ya Usiku wa Mshike Mshike inapigwa usiku wa leo alhamisi Oktoba 27,2016 kuanzia saa moja jioni. Atakuwepo Malikia wa Taarabu, Khadija Omar Kopa, pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic na Fatina Khamis kutoka bendi ya Big Star.

Kabla ya saa tano usiku utalipa shilingi 7,000 tu na shilingia 10,000 baada ya saa tano usiku. Burudani kali itadondoshwa na #LakeFmDjz Mwanza kama matangazo yanavyoonesha.
Na BMG


Bonyeza HAPA Kujua Zaidi

RPC KINONDONI ATOA TAHADHARI KWA WAMILIKI WA MAGARI JIJINI DAR ES SALAAM

RPC Suzan Kaganda

Na Dotto Mwaibale

WAMILIKI wa magari wametakiwa kuchukua tahadhari ya kuzima na kufunga milango magari yao pale wanaposimama kwa dharura kupata mahitaji mbalimbali ili kuyanusuru kuibwa.

Mwito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Suzan Kaganda wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu tukio la kuibwa kwa gari la Kapteni Innocent Dallu maeneo ya Mbezi Juu huku akiwemo mtoto wake Lightness.

"Napenda kutumia fursa hii kuwaomba wamiliki wa vyombo vya moto kuchukua tahadhari ya kuzima magari yao na kufunga milango wanaposimama maeneo yoyote kupata mahitaji yao kwani si rahisi kumbaini mhalifu kwani wapo kila sehemu" alisema Kaganda.

Alisema katika tukio la kuibwa kwa gari la kampteni Dallu alikuwa amesimama maeneo ya Mbezi Juu bila ya kulizima akinunua mahitaji ambapo walitokea vijana wakaondoka na gari hilo aina ya Toyota Harrier baada ya kumtelemsha mmoja wa watoto aliyekuwemo ndani ya gari hilo aitwaye Philip huku wakiondoka na mdogo wake Lightness.

Alisema watuhumiwa hao walimtelekeza mtoto huyo maeneo ya Golden Bridge katika baa moja na kisha kuondoka na gari hilo ambalo lilipatikana baada kukamatwa na polisi Kiwangwa mkoani Pwani ambapo  kijana mmoja Ezekiel Daud anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.

Alisema ni vizuri wamiliki wa magari kuzingatia jambo hilo ili kuepusha matukio kama hayo ambayo yanapoteza muda mwingi wa kuyatafuta kwani tukio kama hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Kinondoni ambapo wahalifu waliweza kuiba gari aina ya Noah lililosimamishwa bila ya kuzimwa na kuondoka nalo na alijapatikana mpaka leo hii.